Ni vipi vigezo vya mji kuwa jiji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni vipi vigezo vya mji kuwa jiji?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Freddy81, Nov 11, 2009.

 1. Freddy81

  Freddy81 Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Habari wana JF,
  Ninachotaka wandugu ni kuwekana sawa. hivi ni vigezo gani vinavyotumika hapa Tanzania kuifanya baadhi ya miji kuwa majiji?
  Vigezo ninavyovijua mimi ni:-
  1.Idadi ya watu
  2.unachangiaji katika pato la taifa
  3.Miundo mbinu ya kutosha,
  4.Upatikanaji wa huduma za jamii..Afya,maji safi n.k
  5.Maendeleo ya wananchi wake
  Sasa najuliza,kwa mfano wa hili la miundombinu na Huduma za jamii ni kweli huwa linazingatiwa uu ni siasa tu? Kweli kuna baadhi ya Miji kam Mwanza inakua kwa kasi, Lakini Je Vipi kuhusu Jiji la Tanga, Jiji la Mbeya na Arusha kama sikosei nalo ni jiji.
  Mnazungumziaje na jiji letu Kongwe kabisa la DSM je lina Miundombinu ya Kutosha na mizuri? Nadhani ndo jiji linaloongoza Duniani kwa kujengwa ovyo..

  Je ni vigezo vyote hutumika au kikiwepo kimoja kati ya hivyo ndo imewin???? Au ni kamchezo ka siasa tu. Embu tuwekane wazi kuhusu hili wandugu.
  Ni Hayo tu
   
 2. Freddy81

  Freddy81 Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau mbona kimya?
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mada yako haina mvuto! Ila kuna vimiji vingine Bongo vimepewa hadhi ya jiji kwa sababu za kisiasa! Mfano Mbeya, yaani mji watu wanalala saa 10 jioni, hamna hata klabu ya usiku ya maana eti nalo ni jiji! Phew!!!
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi Arusha na Mbeya wapi pana staili kuwa JIJI?
   
 5. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Bora Arusha! Pako laivu zaidi na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa!
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  basi kale kamsemo cha watanzania tumerogwa! Kanazidi kukolea ! Wahusika wabadili mitazamo yao
   
 7. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Je mnafahamu kuwa na Moshi iko mbioni kuwa jiji? Uongozi wa Manispaa katika malengo yake ya miaka 10 ijayo ni kuwa Moshi ipate hadhi ya jiji, ukifika ofisi za manispaa pale Moshi kuna bango kubwa limeandikwa malengo yao. Na kwa kweli, kwa waliofika Moshi zamani, wakienda sasa hivi kuna tofauti kubwa
  1. Mji wa Moshi toka zamani ulipangika vizuri, una mitaa ya kueleweka, alternative routes kibao
  2. Mji ni msafi
  3. Huduma za jamii za kueleweka: maji (ni nadra sana usikie eti eneo fulani Moshi halina huduma ya maji), barabara sasa hivi kwa kiasi kikubwa ni lami safi, ile tabia ya mji kwenda kulala baada ya saa 11 haipo tena, sehemu za starehe kwa wingi (kinachosubiriwa sasa ni jumba la sinema ambalo nimesikia linafunguliwa siku za karibuni) nk
  4. Vyuo kwa wingi: KCMC, MUCCoBS, Mwenge, Mweka, Sebastian Moshi etc... hivi vimechangia sana kuongeza idadi ya wakaazi na kuuchangamsha mji, pia magari (not necessarily an indicator of progress/ development) yameongezeka na sasa hivi si tu zile 504 na pickup zilizozoeleka zamani

  Kilichobaki sasa ni viwanda vingi vilivyokuwepo zamani kufufuliwa baada ya kufa katika ka-mchezo fulani ka kuwaadhibu wenyeji baada ya kusapoti upinzani!!
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Injinia ni MOSHI kuwa jiji au KILIMANJARO kuwa jiji???
   
 9. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ha ha!! Ni Moshi bwana. Mi sijui kuhusu Kilimanjaro nje ya Moshi. Kwa nini umeuliza hivyo? Nilidhani nilichoandika ni kuhusu mji wenyewe wa Moshi
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa jumla miji inayo stahili kuwa na sifa ya jiji Tanzania ni DAR, Mwanza na Arusha tu.
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Unaweza kwenda kuuliza TAMISEMI watakupatia sababu. Lakini lazima ujue kuwa hakuna vigezo vya kimataifa juu ya hadhi ya miji. Hivyo usilinganishe na nchi za wenzetu. Kwa Tanzania kuna sababu za kisisa pia katika kuipandisha hadhi miji.

  Kwa mfano Mwaka 2005 lilipitishwa azimio kwamba miji yote ambayo ni makao makuu ya mikoa iwe kwenye ngazi angalau Manispaa. Hivyo Mikindani-Mtwara, Lindi, Ujiji-Kigoma, Songea, Rukwa nk ukapandishwa hadhi toka miji kuwa manispaa. Hivyo kigezo kikubwa ilikuwa ni makao makuu ya mkoa na si vinginevyo.

  Mbeya na Mwanza pamoja na vigezo vingine, zimepandishwa toka manispaa kuwa jiji kutokana na kuwa makao makuu ya kanda ya kusini na kasikazini respectively (siyo rasmi). Ninamaanisha kwamba ktk Tanzania kuna kanda licha ya kwamba hazipo rasmi. Miradi au shughuli za Serikali zinazosimamiwa kikanda. Nadhani na Arusha inaingia hapa ila sijui kuhusu Tanga.
   
 12. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Hapo natofautiana na wewe Magezi. Arusha!! Ile vurugu nayo ni jiji? Ni kwamba tu ina vitu vichache vinavyotakiwa katika jiji lakini the main thing kwa mfano lay-out ya mji (it was originally planned as a small hunting town), huduma ya maji safi na maji taka (you might argue kwamba mbona Dar ni jiji).

  Usidanganyike na majengo machache marefu, wingi wa watu (tena wenye hela), uzuri wa magari, viwanja vya starehe nk. Jiulize, je UNICTR wakiondoka Arusha leo, mzunguko wa pesa utakuwa sustained?
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Namaana kwamba , Badala ya kuita Jiji la Dar basi wangeita Jiji la K'ndoni au Ilala Injinia
   
 14. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Arusha kuwa jiji bila UNICTR inawezekana mkuu, UN-ICTR ni kigezo cha sehemu tu ya mzunguko wa mapesa A-city Mkuu
   
 15. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Oh, ok, nimekupata Kimbweka. Nadhani waliokosea ni walioupa mkoa jina la Dar-es-Salaam kwani kilichoanza ni mji/ bandari ya Dar-es-Salaam, hivyo jiji linastahili kuendelea kuitwa kwa jina hilo ila tu mkoa ndio ungetafutiwa jina lingine kama vile "Mkoa wa Ngereko" au kitu kama hicho
   
 16. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Usinipate vibaya. Mimi mwenyewe Arusha ndio kwetu. Ila kwa kweli hadhi ya jiji haistahili. This is my personal opinion. The TOWN is so disorganized, dirty, cramped...to mention a few negatives. Sikatai kwamba kuna mambo mazuri pale, ila kwa jinsi ulivyo sasa hivi, hapana. Labda wafanye mpango wa kuupanua (jambo ambalo niliwahi kusikia lilipangwa kufanyika ila wenyeji (Waarusha) waligoma kuachia ardhi zao hasa katika maeneo kama Kijenge, Moshono, Njiro chini, Sekei etc) na kuongeza barabara + alternative routes.

  Kwa kifupi kwa mawazo yangu Arusha ni jiji only in terms of the lifestyle of it's residents!!
   
Loading...