Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,129
- 18,743
Kuna wakati najiuliza kati ya wanasiasa na wapiga kura ni nani ana kumbukumbu fupi zaidi. Kwa mfano, wakati fulani kulikuwa na kampeni ya kubomoa nyumba bila kulipa fidia hapa Dar, na wananchi wote wakalaani sana kitendo hicho.
Hivi katika wale waliolaani kitendo hicho ndio walewale tunawashudia wakiwa mbele kwenye kampeni za CCM, au wale kule Bukoba waliopata maafa wakaambiwa watajiju wenyenyew, leo wako wapi katika suala la CCM Vs Chadema? Au Watanzania kwa ujumla, waliposikia kauli kwamba wakazi wa Mwanza hawatabomolewa nyumba kama wakazi wa Dar kwa kuwa walimpigia kura mgombea wa CCM, hii inawapa msimamo gani katika kampeni za CCM Vs Chadema?
Au tuliposhuhudia wimbi la utekeji watu na waandishi wa habari wanaoikosoa serikali na viongozi, na hata mauaji yao, na kila mtu kulaani kwamba serikali haichukui hatua huenda hata inahusika, leo watu waliolaani vitendo hivi wako wapi katika suala la kampeni hizi?
Au wafanyakazi kwa ujumla, walipolaani sana suala la kikokoto cha mafao na kikaahirishwa hadi baadae (sijui lini), au pale wanaponyimwa nyongeeza za mishahara ili fedha ya ndani itumike kwenye miradiwanakuwa wapi katika suala nzima la kampeni za CCM Vs Chadema?
Nina mifano mingi lakini hii inatosha. Je, ni nani anakuwa na kumbukumbu fupi katika masuala kama haya, ni wapiga kura au wanasiasa wanaorudi kutuomba kura?