Ni vipi pombe aina ya ulanzi tunaweza kuiweka katika vifungashio ili kuuza na kusambaza nchini na dunia nzima?

zinginary

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
2,467
1,686
Habar ya asubuhi wakuu??

Hapa nililala na ndio nimeamka but kuna kitu kichwan kinatesa since Jana

Jana jion nikiwa mizunguko yangu nikakutana na watu katika machimbo yao kadhaa wanajivinjar pombe aina ya ULANZI hiyo ni pombe maarufu sana iringa

Nipo Mbeya kwa sasa hawa jamaa wananunua Lita moja kwa sh500/= hii ni natural product kabisa na hii pombe ikilala inakuwa na ukakasi flan na nichungu wanaita(MKANGAVU) SO BAADA YA KULALA WANYWAJI WENGI WANAKUWA HAWAIPENDI, yaan in short hii pombe inapendwa iliyo GEMWA leoleo inakuwa tamu ni nzur nk..

Hii aina ya pombe ni huwa mala nyingi inapatikana kipind cha kifuku Tuu,kiangaz huwez kuipata au ukipata kwa uchache na kwa Bei ya juu kabisa hiyo ni kwasababu ya uhaba wa technologia jinsi ya kuistore..na pia inapatikan kwa wingi nyanda za juu kusini maana hata wakigema Leo makete Mbeya mjini na maeneo mengine itafika leoleo bila kuchacha kuwa mkangavu..so na ndio mana kwa tz pengine hii pombe ni maarufu kwa hii kanda Tuu

Kwasababu HIZO nikaa na kufikiria usiku kwann tusiiweke ktk package ili I we inauwezo wa kuuzika hata kiangazi na pia iwe na uwezo wa kusambazwa nchi nzima na iwe kma kinywaji maarufu cha asili kama ilivyo Korea ( SOJU NA RICE WINE)

WATU mliosoma fermentation mtakuwa deep sana na kuelezea kwann inachacha na kwann hatuwezi kuiweka ktk chupa na vipi itawezekana..??

By the way

Kule iringa wakigema huwa wanachimbia chini na haichachi sasa navyo Jua hicho ni kitendo cha kuiweka mbali na oxygen (ktk fermentation kuna mambo ya anaerobic na aerobic) ndivyo wanavyo Fanya bila wao kujua nimeamka usingiz na kaidea haka next time nikitulia na kuifanyia utafiti nitakuja na wazo but now kwayeyote kwenye uzoefu unaweza to a wazo lolote na watu wakafanyia Kaz..

Wabongo wengi wanaizarau kuwa ni Mataputapu,local nk but IPO day wataiheahimu kama wanavyo heshimu honey wine..

Nawasilisha na ngoja nikafungue lock

Asubuhi njema
 
Aisee hii pombe mkuu nikiboko ni balaa tupu moto wakuotea mbali wazo zuri kabisa tunaikosa kiangazi wengine wanaiita "kiteta"
 
Aisee hii pombe mkuu nikiboko ni balaa tupu moto wakuotea mbali wazo zuri kabisa tunaikosa kiangazi wengine wanaiita "kiteta"
Yeah na pia kuna baadhi ya mikoa Hapa tz hawaijui kabisa hiyo ni kwasababu mpk kufika mkoa mmoja had mwingine kwa mzigo ni km siku2 na kuendelea
 
Yeah na pia kuna baadhi ya mikoa Hapa tz hawaijui kabisa hiyo ni kwasababu mpk kufika mkoa mmoja had mwingine kwa mzigo ni km siku2 na kuendelea
Huu mzigo udumu milele aisee nilikua nauchukulia poa sana watu wengi hawaupati huu ila wachache wambeya na iringa umetoa wazo zuri sana mkuu
 
Mkuu, kidogo nikurekebishe,
Ulanzi stimu au % za alcohol huongezeka kadri muda unavyoenda, ikitoka kugemwa tu huwa mtogwa ukikaa ndo alcohol huongezeka, sasa ikilala kwa mabingwa ndo hupenda zaidi maana stimu zinakuwa zimeongezeka ili kukata uchachu huchanganya naulanzi mpya yaani wa leo unachanganywa na wa jana.
Kwahiyo ulanzi una hatua tatu...kuna mtogwa...mkangafu na mdindifu...
 
Huu mzigo udumu milele aisee nilikua nauchukulia poa sana watu wengi hawaupati huu ila wachache wambeya na iringa umetoa wazo zuri sana mkuu
Asante mkuu

Ngoja tuingie ktk tafit kila kipind kijacho tuweze kuwafikishia wakinga na wasafwa nk waliopo mbali na kwao kwa muda mrefu
 
Mkuu, kidogo nikurekebishe,
Ulanzi stimu au % za alcohol huongezeka kadri muda unavyoenda, ikitoka kugemwa tu huwa mtogwa ukikaa ndo alcohol huongezeka, sasa ikilala kwa mabingwa ndo hupenda zaidi maana stimu zinakuwa zimeongezeka ili kukata uchachu huchanganya naulanzi mpya yaani wa leo unachanganywa na wa jana.
Kwahiyo ulanzi una hatua tatu...kuna mtogwa...mkangafu na mdindifu...
safi mkuu umetoa Maelezo mazuri uko vizuri mkuu ukilala huu ndo wataalamu wanauelew ila wengi wanapenda kiteta ulotoka kugemwa maana nimtamu sana sio kitoto
 
Nalitambua hilo mkuu,

Pombe ikilala ndio alcohol inakuwa juu

Sasa hii mada nimeleta ili wataalamu waje,maana nacho taka hata ikilala iendelee kuwa na radhaa ileile kama mwanzo

Na ndio mana nikatolea mfano hapo chini kuwa kule makete huwa wanafukia chini

Waliosoma fermentation watakuja na jibu ya jinsi ya kumaintain flavour hata alcohol per ikipngezeka au hata mie baadae naweza toa jibu nzur
 
safi mkuu umetoa Maelezo mazuri uko vizuri mkuu ukilala huu ndo wataalamu wanauelew ila wengi wanapenda kiteta ulotoka kugemwa maana nimtamu sana sio kitoto
Yeah mkuu wale wababe ndio wanapenda ulio lala ila tunahitaji kuweka product zote aina tatu kama alivyo sema mshikaji juu

Ila unao uzika sana ni waleoleo
 
Mkuu mimi ni mtaalam wa Pombe, napenda kuchangia hapa.

Kwanza niseme hiyo pombe siijui, ila huwa naisikia kwa rafiki zangu wa Iringa.

Kutokana na maelezo yako, umesema pombe hiyo haipaswi kulala, ikisha gemwa basi lazima itumike siku hiyohiyo.

Ulanzi ni pombe inayotokana na Mmea unaoitwa Mlanzi.

Wakazi wa Iringa hukwenda kuchimba vishimo kwenye mmea huu na kesho yake hukuta vishimo vimejaa maji ambayo ndio pombe yenyewe.

Bila hata kuuona mmea wenyewe, lkn kwa maelezo hayo basi naweza kuelewa nini kinachofanyika.

Ni dhahiri kwamba Mmea huo ukichimbwa kishimo kwenye bua (stem) hutiririsha maji kutoka kwenye misuli yake kutoka juu na mengine kutoka chini.

Kwa wale mliosoma biology mnatambua jinsi mmea unavyosafirisha chakula na maji kupitia xylem na phloem. Hii ni kama mishipa ya mmea.

Mishipa hii ukiikata ni kama vile umekata mshipa wa damu, yani lazima damu ivuje.
Kwakua wagemaji hawa huchimba kishimbo ndani ya bua hili basi chkula cha mmea ambacho hutebgenezwa kwenye majani na kusafirishwa sehem mbalimbali za mwili huvujia katika kishimo hiki kupitia phloem (mshipa wa kusafirisha chakula). Pia maji ambayo hutokea chini yaliyofyonzwa na mmea huu kupitia mshipa wa xylem huja kujaa katika kishimo hicho.

Kumbuken kwamba Mmea hutengeneza chakula chake kupitia majani. Na moja ya chakula hicho ni glucose, sucrose. Chakula hiki kikisha tengenezwa ndio huvunjwa na kutengeneza nishati ya mmea ambayo husaidia kuendelea kuishi.

Sasa Kipindi wanapochimba kishimo ndani ya bua la mmea huu, chakula na maji ya mmea hujaa hapo.

Sasa Je pombe inatoka wapi hapo??

Ili pomve ipatikane ni lazima pawe na vitu vikuu vitatu.
Kwanza ni Yeast (amira) pili ni Sukari (glucose, sucrose) na tatu ni maji.

Yeast au amira ni wadudu aina ya fung ambao huigeuza sukari au glucose kuwa ethanol (pombe).
Kuna Yeast wa mwituni au msituni (wild yeast) ambao wanaishi kwenye mimea hasa ile yenye sukari kama miwa, maua ya mmea nk.

Hivyo Yeast ambao wapo kwenye mmea wa Mlanzi, huitafuna sukari ile kwenye hiko kishimo na kuigeuza kuwa ethanol/pombe, na kiasi kidogo sana cha methanol (sumu).

Sasa, Je ni Kwanini Pomve hiyo ikilala inaharibika au kuwa kali sana na kusababisha Hangover?

Kwa kawaida ethanol ambayo ndio kilevi chenyewe ikikutana na hewa (oxygen) hugeuka na kuwa Ethalyene (acetaldehyde) na kile kiasi kidogo cha methanol hugeuzwa kuwa formaldehyde .

acetlaldehyde na formaldehyde hizi ndizo husababisha Hangover, kichwa kuuma, kizunguzungu, mdomo kukauza, kuchoka, misuli kuuma nk

Ndio maana kwa maelezo yako unasema ikisha lala hugeuka kuwa Mkangavu ambao wengi hawaipendi.

Ndio maana Pombe ukisha ifungua na kuiacha wazi kwa muda mrefu huruhusiwi kunywa. Hata kwa wale wa Moshi wanaijuia Ngera/ Ngira ambayo ni mbege iliyolala

Shukrani.
 
Nikiwa Iringa pale maeneo ya wilolesi maarufu kwa kuosha magari nilijumuika na wazee kwenye mzunguko na kupasiana ulanzi.... Ni pombe tamu na inayolewesha taratibu huku magoti yakikosa nguvu taratibu mno mpaka unapojishtukia huwezi kusimama dede.....
Ulanzi ni kama ilivyo CHIBUKU pride of Tanzania...
 
Back
Top Bottom