Ni vipi nitapata haki yangu ya kumilikishwa mali nilizochuma na mume wangu?

Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,351
0
Nimeish na mume wangu miaka 11,wote tulikuana hatuna uwezo,tukaanza maisha pamoja,mimi nilikua nimeajiriwa nauza duka na yeye dereva,Badae niliacha kazi kulea mtoto wetu wa kwanza,Yeye aliendelea na kazi na mimi nikaendelea kumshauri afanye maendeleo,tukajenga,tukafungua miradi,Tukanunua gari 3.Badae nikajiajiri kwa kufungua duka letu,Kumbe mwenzangu kazaa nje na kudhamiria kuniacha mimi ili aoe huyo mwanamke wkt kwa sasa tayari nina mtoto mwingine wa miez kadhaa,Alichofanya yeye ili ahakikise sipati kitu ni KUBADILISHA HATI ZA MALI ZETU ZOTE NA KUANDIKA JINA LA MTOTO WANGU MDOGO, je baada ya ndoa kuvunjika nani atasimamia hizo mali ni mimi au yeye? Na je baada ya ndoa kuvunjika, kisheria naruhusiwa kudai kumilikishwa mali kwa jina langu na si la mtoto?NISAIDIENI JAMANI
 

NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
860
500
Kuna taasisi mbalimbali zinaweza kukusaidia kuna Tanzania Gender Network Programme(TGNP). Na hata TAMWA. Jaribu kuulizia ofisi zao. Hao ni Wanaharakati wanawake ambao watakusaidia sana. Kwani wamesaidia wengi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom