Ni vipi naweza kupata Mwekezaji kwenye kiwanja changu cha Biashara?

Kenney

JF-Expert Member
Dec 8, 2013
294
165
Habarini say Asubuhi wadau wote wa JF hususan wabobezi katika hii. kona maalum ya Uchumi, Kama kichwa kinavyojieleza, nimekuwa nikiona vitega Uchumi vingi katikati ya mji (kwa maana ya majengo ) ambayo mengi nasikia kuwa hujengwa na makampuni fulanifulani kwa mikataba maalum na wenye plot husika, swali langu hapo ni kwamba iwapo nina eneo ambalo lipo eneo zuri la kibiashara na sina uwezo wa kuliendeleza ila nahitaji wawekezaji wa aina hiyo ni hatua gani natakiwa nichukue au utaratibu gani wa kufanya ili na mimi nikabahatika kupata hilo zali! Sijui kama nimeeleweka? Naomba kuwasilisha!
 
Kama ulivyosema "zali" mkuu huwa halina plan. Huwa linakujaga tu kubum kabam


Otherwise kama sehemu ina potential unaweza mwenyewe kutafuta hao wawekezaji na kuwashawishi wakatumia eneo lako na ukaingia nao mikataba.

Ngoja wanauchumi waamke watakupa majibu mazuri zaidi.
 
Naangalia uzi... Nina eneo kama hilo na linafaa hostel... Lipo Moshi.
 
Back
Top Bottom