Ni vipi mtu anaweza kujua jina la mmiliki wa gari kupitia plate number?

Mwita Mtu Mrefu

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
740
1,106
Hello JF,

Naomba kujua ni kwa namna gani naweza kumtambua mmiliki wa chombo cha usafiri hususani gari bila purukushani za kwenda polisi.

Je, inawezekana kupata taarifa online? Majina, namba za simu?
 
Na mimi naongezea, naomba kuweza kujua jina la mmiliki wa leseni kwa kutumia namba ya leseni.
 
Hello JF,

Naomba kujua ni kwa namna gani naweza kumtambua mmiliki wa chombo cha usafiri hususani gari bila purukushani za kwenda polisi.

Je, inawezekana kupata taarifa online? Majina, namba za simu?
Taarifa hizi ni za siri sidhani kama kwa Tanzania ni publicly available.
 
Mpaka uwe ndani kitengo au uwe na mtu ila mtu wa kawaida huwezi hakuna system inayiruhusu hvo
Mimi nimeuliza hili swali kwakuwa,gari langu lina faini nimeshakamatwa na trafic mara 2,inaonekana ili zidisha speed,eneo ambalo hata mimi silijui,ila leseni iliotumika sio yangu ,wala mtu yoyote nyumbani kwangu,na muda inayoonekana hilo kosa lilifanyika gari nilikuwa nayo mwenyewe...
 
Zile plate namba mfano T 990 BQJ ukiweka kwenye system unakutana na jina lako ....

Hio system nimeiona bandalini..
 
Mimi nimeuliza hili swali kwakuwa,gari langu lina faini nimeshakamatwa na trafic mara 2,inaonekana ili zidisha speed,eneo ambalo hata mimi silijui,ila leseni iliotumika sio yangu ,wala mtu yoyote nyumbani kwangu,na muda inayoonekana hilo kosa lilifanyika gari nilikuwa nayo mwenyewe...
Nenda trafiki peleka lalamiko litashughulikiwa, ila itataka uvumilivu.
 
Mimi nimeuliza hili swali kwakuwa,gari langu lina faini nimeshakamatwa na trafic mara 2,inaonekana ili zidisha speed,eneo ambalo hata mimi silijui,ila leseni iliotumika sio yangu ,wala mtu yoyote nyumbani kwangu,na muda inayoonekana hilo kosa lilifanyika gari nilikuwa nayo mwenyewe...
Hapo maana yake kuna gari lingine lina namba kama yako. Nenda TRA utashangaa kukuta gari lako limeondolewa kwenye usajili na linalotambulika ni hilo lingine lililosajiliwa kimagumashi. Mara nyingi ni yale magari watu wanakopea benki.

Kingine angalia Eneo ilipopigwa fine gari na jina la askari kisha muone ofisini kwake umueleze hilo, itakurahisishia kupata ufumbuzi

Mwisho angalia TIRA mis kujua gari iliyowekwa bimani ni ya kwako au hilo lingine. Kama liliwekwa ni lingine, angalia jina la kampuni ya bima nenda ofisini kwao waeleze utapata jina mpaka na namba ya simu ya mmiliki mwenza halafu mtaulizana wenyewe.
 
Taarifa binafsi za mmiliki wa chombo cha moto zilikuwa publicly available kwa kutumia plate number miaka ya nyuma kupitia website ya TRA lakini ilikuja kuondolewa kimya kimya na serikali.
 
Nenda ofisi ya bima yoyote ongea nao vizuri watakupa taarifa unayohitaji Wanayo hiyo system
 
Back
Top Bottom