Ni vipi Elimu ya mama inaathiri ufaulu wa mtoto shuleni?

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Ripoti ya Uwezo inayotoa Tathmini ya hali ya kujifunza nchini inasema kuwa watoto wenye mama mwenye elimu ya sekondari au zaidi wanafaulu zaidi ya wale ambao wazazi wao hawajasoma.

Screenshot from 2017-04-28 12-50-15.png


Napata shida sana kuelewa hii 'concept'. Mtoto anaenda shule na kujifunza, anarudi nyumbani na kula, kucheza na kulala tu. Sasa iweje elimu ya mama iathiri ufaulu wa mtoto? Na iweje mama tu, baba je?

Je ni kwa sababu mama kama ameelimika atasaidia kufundisha mtoto akiwa nyumbani?

Au ni kwa sababu kama mama ameelimika ina maana na baba ameelimika hivyo wana uwezo fulani wa kumpa mtoto wao elimu ya kiwango cha juu?

Naomba walimu na wadau wengine wa elimu tujadili.
 
Uwezo wa kutia moyo ni mkubwa kwa mtu anayejua unachokifanya,na mama yuko na hiyo fursa zaidi kumtia moyo mtoto wake,lakini pia hata kama anakazi nyingi vipi huwa hakosi muda wa kujua kuhusu kile mwanaye anafanya na changamoto anazopotia. Upande wa baba ni mtafutaji zaidi,ukila na kuvaa na ada ikalipwa basi.
 
ufaulu ni matokeo ya mazingira na asili.


mazingira ni pamoja na ngazi ya elimu ya watu wanaomzunguka, jamii na mtazamo wa elimu, miundombinu ya shule, Sera nk.


asili, urithi wa maarifa toka kwa wazazi.
 
Back
Top Bottom