jd41
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,756
- 4,842
Wakuu Salaam.
Kuna watu wanaodai wapo neutral kwenye siasa, kwamba wao hawana upande. Wamekuwa wakirudia kauli zao mara kwa mara kujaribu kuuaminisha umma wanachokisema ni sahihi, japo ni ngumu sana kukipeleka kwenye practical (kiuhalisia).
Hasa ukizingatia kwamba, maisha ya mwanadamu wa kawaida yametawaliwa na hisia kwa kiasi kikubwa, hivyo mtu huweza kujikuta amependa au kuchukia upande fulani, sio tu kwasababu ya kile wanachofanya, bali pia inawezekana mtu akaupenda upande huo kutokana na kupendezwa na mtu fulani aliyepo upande huo.
Hivyo automatically, utapompenda mtu huyo wa upande fulani, ni rahisi sana kujikuta umeangukia upande huo bila wewe mwenyewe kujijua.
Lakini pia, kwenye upande wa waandishi, ili uwe neutral kwenye siasa, jambo la msingi kabisa, ni lazima uhakikishe kwa kila hoja unayoizungumzia, lazima uguse pande zote mbili; mfano: kama jambo fulani limetokea ikaonekana upande mmoja umeonewa na upande mwingine, liseme wazi bila kusita, at the same time ukiutaka upande wa pili kuacha matendo, yake maovu kwa upande ulioonewa, na kinyume chake.
Hili linahitaji ujasiri wa dhati, ili ufanye hivyo sharti la kwanza ni lazima uwe tayari kuonekana mbaya na upande utakaoulamu. Hivyo, kwa mfano upande unaoulaumu ndio wenye nguvu ( polisi, bunge) utajikuta unaogopa kuukemea wazi kwa matendo yake mabaya kuogopa adhabu yao.
Mara nyingi utajikuta unakuwa na tabia ya kun'gata na kupuliza; lakini kwenye siasa hilo ni gumu kutendeka kwasababu matukio yanayotokea yanaonekana wazi, zuri linaonekana, na baya linaonekana pia.
Wakati wewe ukijaribu kuficha lile baya la upande wa wenye nguvu, wengine kwa upande wao wanakuwa tayari walishaliona, hivyo regardless ya chochote utachoandika, watakuwa tayari wanaujua ukweli.
Ni rahisi sana kuegemea kulaumu upande mmoja zaidi kwasababu kwanza; hawa hawana cha kukufanya zaidi ya kelele tu za wapenzi na wanachama wake, pili; kuufurahisha upande wa pili, ambao ndio wa wenye nguvu.
Hivyo, mtu au watu wa aina hii, wanaojinasibu wako neutral, hujikuta wanakosa uhuru wa kuandika ukweli na kujikuta wamefungwa kimawazo, either kwa kujua au kutojua, wataandika yale wanayoamini hayatawasababishia matatizo, na hii ni nature ya kibinadamu, siku zote tunahitaji kuwa sehemu salama, tujihisi salama (kimawazo na matendo).
Matokeo yake hili huondoa ile dhana ya mtu kudai kuwa neutral, mara nyingi utajikuta unaendelea kuegemea kulaumu upande dhaifu, ili kujihakikishia usalama wako.
Sent using Jamii Forums mobile app