Ni vigumu sana kuwaamini wana siasa

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Wanasiasa wa nchini kwetu Tanzania wapo kimaslahi zaidi wanachoongea ni tofauti sana na wanavyokiamini, wamekuwa wakiongea hoja nzuri ili hali wao hawawezi kutekeleza hoja zao nitatoa mifano miwili tu.

Mheshimiwa Humprey Polepole alipinga sana uwepo wa wakuu wa wilaya, alisema hawana kazi, Ni matumizi mabaya ya fedha za watanzania, na akijinasibu Tanzania inasehemu nyingi zinahitaji pesa na si kuwapa wakuu wa wilaya ambapo hawana kazi yeyote.

Mheshimiwa magufuli Alimchagua polepole kuwa mkuu wa wilaya, kwa mujibu wa polepole wakuu wa wilaya hawana kazi ya kufanya yeye akakubali kuwa mkuu wa wilaya na kuchukua pesa ambazo alikuwa anazungumzia zipelekwe kwenye maendeleo ya wananchi. Kumbe mkuu wa wilaya ana kazi ya kufanya ukichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya usipochaguliwa mkuu wa wilaya hana kazi maneno hayaaaaa.

Pili Prof mkumbo alilaani kitendo cha Rais kuteua watu toka chuo kikuu cha udsm kwa kuwa chuo hicho kinakabiliwa na ukata wa wahadhiri na alinukuriwa akimwomba Rais aache kuteua wahadhiri hao cha kushangaza baada ya yeye kuteuliwa kuwa katibu mkuu wizara ya mJi na umwagiliaji ameshukuru na kumpongeza mheshimiwa Rais.

Ombi kubwa kwa wana siasa wa Tanzania kusimama kwenye maneno yao, unapoongea kitu fulani na kukataza kitu fulani na kesho unafanya tofauti na maneno yako ya Awali inafanya siasa ionekane kama ni uongo kumbe si maana wala dhana nzima ya Siasa. SIASA ZA BONGO POYOYO NYINGI KULIKO MATENDO
 
Back
Top Bottom