Ni vigumu kuamini....: Zanzibar haina umeme kwa zaidi ya mwezi sasa.

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Nimekuwa hapa Unguja toka Alhamisi. Nimekuta hakuna umeme na katika uliza uliza yangu nimeambiwa kuwa hakuna mategemeo ya kurejesha umeme hadi mwishoni mwa mwezi Februari. Inawezekana serikali inafanya jitihada kutafuta ufumbuzi lakini ni vigumu kuamini kuwa hili tatizo linahitaji miezi zaidi ya 2 kulitatua.
 
Mtegemea cha nduguye hufa maskini. Nguo ya kuazima haisitiri makalio! Naona ndio maana wamehamua kushughulikia matatizo yao ya nyumbani, ili waweze kukabiliana na haya matandiko ya kuazima. Ivi huko baharini si pia kuna upepo daima? nadhani hawahitaji umeme wa mtera, halafu wakipata hata hivyo vichupa viwili vya mafuta wanaweza kuondokana na hii kadhia!

Nawapongeza kwa kuweza kuelewana wao kwa wao kwanza kwani maslahi yao sasa yatakuwa mbele. Nadhani hata lili swala la kuchaguliwa rais chimwaga litakuwa limefifishwa kwa kiasi kikubwa
 
Nono, una maana kuwa suala la umeme kwa Wazanzibar siyo top priority kulinganisha na hili fumbo la muafaka/maridhiano?
 
Ngoja mkione cha moto na bado. mbona Dar.Arusha.Mwanza.Mbeya,Kilimanjaro hadi vijijini umeme upo. kwani kwenye hii miji ndipo umeme unazalishwa? tanesco walikuwa wapi? kwani wazanzibar wanatumia umeme bure?
Enyi wazanzibari inabidi mtambue kuwa mbaya wenu ni Tanganyika na viongozi wenu mamluki.
 
Nono, una maana kuwa suala la umeme kwa Wazanzibar siyo top priority kulinganisha na hili fumbo la muafaka/maridhiano?

Dar sijasema kuwa sio kipaombele kikubwa! Nadhani ungetembelea pemba ungefahamu zaidi. Kwani tangu uhuru pemba mambo yako je? more that 40 years! Mimi naamini wazenj wataweza kutekeleza mengi baada ya kuwa kitu kimoja!

Walikuwa na bahati mbaya kuwa wamekuwa wakigawanywa sana kabla na baada ya mapinduzi. Kabla ya mapinduzi wapemba walikuwa karibu sana na serikali ya waarabu na baada ya mapinzui na waunguja wakajiambatanisha na Tanganyika ili kujilinda. Matokeo yake hata rais wa visiwa hivyo, ni lazima ateuliwe na [Tanganyika]. Hivyo kwa maoni yangu, prioroty za wazenj zilikuwa mara nyingi shaped na bara. Ni mtizamo wangu tu
 
Back
Top Bottom