Ni vigezo vipi vilivyoipa Star TVushindi wa zabuni ya kuonesha Ligi ya VodaCom? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni vigezo vipi vilivyoipa Star TVushindi wa zabuni ya kuonesha Ligi ya VodaCom?

Discussion in 'Sports' started by Balantanda, Dec 13, 2010.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Salama wakuu?...Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza na kuwazua na kujiuliza maswali kibao juu ya vigezo vilivyoipa Star TV mkataba wa kuonesha moja kwa moja michezo ya VPL....Pamoja na kushinda zabuni hiyo Star TV wameshindwa kuoneshwa michezo ya VP iliyochezwa nje ya jiji la Mwanza kwa madai kwamba gari lao la kurushia matangazo haliwezi kusafiri umbali mrefu(kwamba linaenda mwendo wa 20km/h)....Hii ina maana kwamba hawataonesha mechi zinazochezwa nje ya Mwanza,kwamba mechi za Morogoro,Dodoma n.k hazitaoneshwa kwa sababu ya hilo gari la matangazo...

  Ina maana TFF(ama waliopewa jukumu la kupitia zabuni) hawakuliona hili wakati wakipitia zabuni hizi?,ni bora wangepewa TBC ama ITV kuliko hawa wababaishaji wa Star TV......
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Dec 13, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu kibonbo bongo unategemea station gani inaweza kurusha mechi zote live tz nzima.
  mechi zenyewe zinachezwa wakati mmoja
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio kuonesha mechi nchi nzima kwa wakati mmoja...Swali hapa ni ilikuwaje wakapewa mkataba wa kuonesha VPL(ambayo inachezwa mikoa tofauti tofauti) ilhali hawana uwezo wa kuonesha katika maeneo hayo tofauti na wana uwezo wa kuonesha mechi za Mwanza tu???...

  Mara nyingi wameulizwa kwa nini wasiende hata Morogoro(kituo kilichokuwa mna timu nyingi za Yanga,African Lyon,JKT Ruvu,Ruvu Shooting na Mtibwa waliokuwa Manungu) na kuweka kambi hapo kuonesha mechiza VPL...Jibu walilolitoa ni kwamba hawawezi kusafiri kwenda sehemu yoyote nje ya Mwanza kwa wakati kwani gari lao linatembea 20km/h.........Kama sio ubabaishaji ni nini hii
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Dec 13, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tunaweza kulalamika hapa bila kujua pengine wao ndio walioonekana bora kuliko wengine,
  pengine wao ndio pekee walioomba.
  Lakini kikubwa kuliko yote ni kuwa hii ni biashara, kufunga makamera na mitambo ya kurusha live matangazo ni gharama sana kwahiyo wao wanaangalia pia biashara yao
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hapana mkuu....Waliomba ITV,Star TV na TBC1.........Hata kama ni biashara,sababu wanayoitoa Star TV si gharama za makamera mengi....Wao wanasema kwamba gari lao la matangazo(OB Van)haliwezi kufika(let say Morogoro) kwa wakati.....Hii ina maana hawakujiandaa kuonesha mechi hizi kwa Tanzania nzima bali walijiandaa kuonesha mechi zitakazochezwa Mwanza tu(kama Simba wasingeenda Mwanza ina wangeonesha mechi za Toto Africans tu).....Huu ni ubabaishaji babaake
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nimekusoma mkuu
  labda watajirekebisha
   
Loading...