Ni vigezo Gani hutumika kupandisha kodi holela, Nini Msaada wa Serikali kwa Wapangaji?


mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
11,376
Points
2,000
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
11,376 2,000
Kila kukicha wenye nyumba wanaongeza kodi, wenye nyumba za bishara hawa ndio hatari zaidi, hali hii huwafanya wafanyabiashara wengi kuhama hama kila siku. Imefikia hata wenye nyumba kukuuzia ndani kabla ya mkataba kwa ajiri ya tamaa zao. mfano nzuri ni kariakoo, unakuta kamlango mtu analipa milioni moja na nusu kwa mwezi, mpe miezi sita utakuta ameshindwa biashara na watu wa benki washanzunguka kuchukua chao. Mtaa wa kongo frem moja ufikia hata millioni mbili kwa mwezi. swali ni je hawa watu wanazingatia sheria za upangaji, inakuwaje mtu kutoka laki tatu kwa mwezi kupandishiwa mpaka laki 5, Mheshimiwa Makamba Junioralianza vizuri kututetea sijui naye ameishia wapi au naye keshanunua jumba k/koo ili atuumize. Kuhusu mapato hawa jamaa wajanja sana wanachukua pesa kama wanaenda kulipa kodi wanaelewana na watu wa TRA wanawapa no feki, utakuta mkataba anaupunguza kutoka laki tano kwa mwezi mpaka elfu 70 alafu anakupa risti ya elfu sabini tu. Nasisi kwa kuogopa kufukuzwa kwenye frem zetu tunabaki kimya, maana frem zinagombewa kama mpira wa kona. Hali hii imetokana na utitiri wa wamachinga wa kichina, ambao wanamitaji mikubwa sana na serikali yao inawajari kwa kuwapa mikopo nafuu, sio kama kwetu huku ukichukua millioni kumi unaacha laki tano mezani. Hivyo huwafanya wafanyabiashara ndogo kushindwa marejesho kwa mwezi. Serikali kupitia serikali za mitaa ndio wakandamizaji wakubwa kwani hawajui wapangaji wanamatatizo gazi lao la zaidi ni kukusanya fedha ya taka kwani hizo wanamaslahi nazo.
 

Forum statistics

Threads 1,295,998
Members 498,495
Posts 31,230,267
Top