Ni vibaya kujua kinachosainiwa na viongozi wetu?

warea

JF-Expert Member
Jan 22, 2010
244
65
Wanajamii na wataalamu ya mambo ya kimataifa,

Wananchi hawana haki kujua kuhusu mikataba inayosainiwa na viongozi wetu?

Mara kadhaa nimeona picha za viongozi wakisaini mikataba lakini kinachoripotiwa ni mkataba juu ya uhusiano wa kimataifa au mambo mbali mbali.

Mfano halisi ni hii habari MICHUZI: MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASAINIANA MKATABA NA MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA IRAN MAKUBALIANO YA PAMOJA KATI YA IRAN NA TANZANIA

Kuna ugumu gani kusema kuwa kiongozi anasaini juu ya ushirikiano katika kilimo, viwanda, utamaduni au kijeshi?

Hayo mambo mbali mbali hayana jina?

Naamini wakituambia mkataba wa kibiashara umesainiwa kati ya Tanzania na nchi fulani, itawasaidia wananchi kujipanga kufuatilia nafasi za biashara.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom