Ni vema wanasiasa wa upinzani kuhifadhi maneno ili kuepuka kuonekana Ndumila Kuwili; ZITTO KABWE zingatia neno hili!!

MshauriHuru

Member
Nov 30, 2018
61
68
Na Morris Ntuyabaliwe,

Kigoma

Kwa muda mrefu ZITTO KABWE amekuwa akikebehi maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kudai kuwa imejikita katika maendeleo ya vitu na siyo maendeleo ya watu, kwamba Serikali ilikuwa haina haja ya kununua ndege na kufufua shirika la ndege la Taifa (ATCL), kujenga madaraja na barabara, vituo vya afya, ukarabati wa vivuko na meli. Wakati kimsingi twajua kuwa hayo yote yanafanywa na Serikali kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuwarahisishia kujipatia vipato vyao vya kila siku katika shuguli zao za kiuchumi na kijamii.

Jambo la ajabu na kushangaza ni kwamba ZITTO KABWE amekuwa akikebehi ununuzi wa ndege kwamba ni hauleti maendeleo kwa watu. Leo tarehe 11.09.2020 amesafiri na Shirika la ndege la ATCL kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kufanya shughuli zake za kisiasa (kufungua kampeni zake za kuwania ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini) ambazo zinampatia ugali wa kila siku yeye pamoja na familia yake. Suala la kujiuliza ni kwamba kama ndege haziwanufaishi wananchi kwanini ZITTO KABWE amesafiri na ndege ya Serikali, kwanini hajaamua kwenda Kigoma kwa kutumia njia anayoijua yeye, ambayo haijafanywa kwa jitihada ya Serikali.

Kwa kifupi ZITTO KABWE ni ndumila kuwili, siyo wa moto wala siyo baridi, achague upande mmoja la sivyo anaaibika kwa tabia yake ya kulopoka hovyo kuhusu masuala ya kitaifa wakati ukweli na uhalisia na faida ya masuala hayo anayajua kiundani.

Watanzania tuendelee kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano kwa utekelezaji wa maradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha yetu, tusikubali kugawanywa na wanasiasa wanapinga kila kitu kama ZITTO KABWE wasio itakia mema Nchi yetu.
Tuungane pamoja na Rais wetu Mhe.Rais Dkt. MAGUFULI kuendelea kuiletea Nchi yetu maendeleo.

images-13.jpg
 
Ni wakati wa kuitupa ccm mbali na nchi hii hawa watu hovyo kabisa na wameleta utengano mkubwa kati ya watu.
 
Kwani Zito kusafiri na Ndege ya ATCL ndo kupata maendeleo wananchi hata wakati hakuna ATCL mbona precision air ili kuwepo pamoja na fastjet
 
Unapoteza muda wako kutetea ccm ambayo inapumulia mashine za tume na polisi
 
Back
Top Bottom