Ni vema Serikali ya Tanzania ikaweka wazi kama bado iko kwenye Uchumi wa Kati au la

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,655
2,000
Hii ni kwa sababu kipindi wanachopitia raia wake kwa sasa ni cha dhiki kubwa mno , ukichunguza utagundua kwamba Ni vigumu kwa raia wa Tanzania kwa sasa kupata milo mitatu , wengi wanapata mlo mmoja tu , tena saa 10 jioni , na baada ya mlo huo duni , ambao unaweza kuwa mihogo na Chachandu hawali tena hadi siku inayofuata .

FB_IMG_1597733863117.jpg

Kuendelea kujidanganya kwamba nchi yetu imekuwa kiuchumi huku raia wake wakinuka uvundo wa dhiki ni sawa na kujipiga kitanzi wenyewe , wekeni wazi hali halisi ili Dunia ielewe na iweze kuwasaidia hata viroba vya mtama na uwele ili raia wanusurike .

FB_IMG_1577871864627.jpg

Nafuu kidogo iko kwa wafanyakazi , ambao hata wenyewe wanateseka kutokana na kutokuongezwa mshahara wala marupurupu yoyote kwa miaka 7 sasa , huku wengi wao wakihamishiwa Dodoma na familia zao zikibaki DSM au kwingine kokote walikokuwa kabla ya uhamisho huo, kwa hiyo mshahara ule ule ambao haukuongezwa hata senti tano sasa unagawanywa mara 2 kwa matumizi , aliyeko Dodoma apate na waliobaki alikokuwa awali nao wapate , Ikumbukwe kwamba Wafanyakazi wa serikali ya Tanzania hawazidi laki 6 , kati ya wananchi wake ambao idadi yao ni zaidi ya mil 60 .

Mficha maradhi mauti humuumbua
 

Mr. Sound

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
662
1,000
mkuu hata kenya wapo uchumi wa kati bt wananchi wake wanakufa na njaa pia wanapewa msaada wa chakula, hatupaswi tanguliza siasa kwa kila jambo hata kama tunakinzana mitizamo
 

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,553
2,000
Benki ya dunia iliunda njia mpya ya makundi ya uchumi mwaka 2016 baadala ya kutumia makundi kama Developing Countries na Developed Countries.

Benki ya dunia imezitenga nchi wanachama katika makundi manne.

1. Uchumi WA Chini.
2. Uchumi WA Kati WA Chini (tz imo humu)
3. Uchumi WA Kati wa juu
4. Uchumi WA juu
IMG_20211019_174422.jpg

Ambapo GDP per capita ya Tz ni 1159 USD Kwa mwaka 2021.

Hii benki ilifanya hivyo ili kila kundi lipate vipaumbele vinavyostahili.

Kwa sababu wakati walipokuwa wanatumia makundi kama NCHI ZILIZOENDELEA na NCHI ZINAZOENDELEA, Nchi kama TZ na China zilikuwa zinawekwa kwenye mizani Sawa kitu ambacho hakipo Sawa.

Kumbuka China ni nchi inayoendelea.

Sioni hata haja ya kuanzisha Uzi Kwa sababu nchi zote zilizomo kundi la Kwanza na la pili zinafahamika kuwa ni nchi masikini ndio maana ikawekwa makundi Mapya ili kupewa vipaumbele vinavyostahili ikiwemo mikopo nafuu.

Hata nchi zenye uchumi WA Kati WA juu nyingi Pia ni masikini.

Vinginevyo labda thread iwe ni ya propaganda kama jinsi chama tawala walivyokuwa wanafanya propaganda na Neno "uchumi WA Kati"
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,480
2,000
Inasikitisha sana mkuu, asubuhi mtu anakula chai ya rangi na vitumbua, mchana mihogo chachandu, usiku ugali na mchicha. Nyama, kuku, na samaki havishikiki, ni anasa!
 

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
5,355
2,000
Vitu vingine havifai siasa, umeangukia pabaya: kwahio hivo ndo viashiria kwamba hatupo uchumi wa kati, na mnataka kuongoza nchi, kazi ipo apo ufipa, enewei kesi ya mbowe haijaisha atatuambia kama amewatuma kupost izi picha
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,655
2,000
vitu vingine havifai siasa, umeangukia pabaya: kwahio hivo ndo viashiria kwamba hatupo uchumi wa kati, na mnataka kuongoza nchi, kazi ipo apo ufipa, enewei kesi ya mbowe haijaisha atatuambia kama amewatuma kupost izi picha
Bado mko uchumi wa kati ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom