Ni vema Serikali ya Tanzania ikairejesha pia NBC

Wakuu natanguliza salamu za sikukuu , Nikiwa kama Mwananchi wa Tanzania , ninayo haki ya kushauri mambo mazuri yanayopaswa kufanywa na Serikali yangu .

Nimeona na natambua juhudi za serikali za kuirudisha mikononi mwa umma kampuni ya simu ya Celtel , Zain na sasa Airtel waliyouziwa watu wasiojulikana kwa gharama ya kutupa isiyozidi Tsh elfu 10.

Naomba Iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara ambayo mauzo yake yalimtoa machozi Baba wa Taifa Mwl Nyerere ilirejeshwe tena mikononi mwa umma .

Miaka michache huko nyuma tuliwahi kurejesha mali zetu zilizoporwa kama vile Tanesco na TRL , hili pia tutaliweza tu.

Mungu ibariki Tanzania .
NBC iliuzwa na Mkapa, patamu hapo.
 
Mkuu ashasema "sipangiwi la kusema na kufanya na myu yeyote".... Unadhani kwa kiburi alichonacho atakusikiliza kweli?
 
Kwani aliyeiuza kafa??!! Ahojiwe kama kweli hatuna double standards kwenye maslahi ya taifa.
 
Ikairejesha kutoka wapi? Unaambiwa hatufukui makaburi. Halafu na lishirika la chama chetu litalipaje yale mabilioni? Acha uchochezi. Tutakupima mkojo
 
Ona walivyoiuza, benki ya watanzania
Kwa kweli inashangaza, bei walioiuzia
Kisha tukiwauliza, hawana la kutwambia
Kwa Heri baba Nyerere, daima tutakukumbuka
 
Back
Top Bottom