Kuna maswali nahisi huwa yanaweza kukosa majibu ! tunapolalamika kuhusu ubovu wa miundombinu ya barabara hususani hapa jijini Dar es salaam na zaidi kipindi hiki cha mvua. Barabara nyingi zinapata mashimo na pengine kuharibika kabisa na kulazimika kutumia pesa zetu walipa kodi kuzikarabati mara kwa mara badala ya pesa hizo kupelekwa kwenye huduma nyingine za kijamii, Na wakati huo huo napishana na Magari makubwa ya mizigo ama yakiwa na mizigo/container au matupu katika barabara zilizo elekezwa kupita TANI 10 TU. Nani anapaswa kulaumiwa, aliyetengeneza barabara isiyo na kiwango cha kupita gari lenye uzito zaidi ya TANI 10? au anaepitisha gari la uzito huo ? Je ni askari wa usalama barabarani wanaoshindwa kutimiza wajibu wao ama wizara husika kwa kushindwa kuwasimamia wakandarasi au Labda ni sisi Madereva ? kind of confusing !!!!