Ni uzembe wa hazina au serikali ya JK imeshindwa kulipa mishahara?

mazegezege

Member
Mar 11, 2012
27
0
Inasikitisha sana kuona wafanyakazi wa serikali hasa walio chini ya halmashauri wakiwa hawajalipwa mishahara ya mwezi Novemba.sababu zinazotolewa ni kuwa wafanyakazi hawa account namba zao hazionekani na wametakiwa kuzipeleka tena kwenye ofisi ya uhasibu na kwa afisa utumishi.suala hili linaacha maswali mengi yasiyo na majibu!

 1. Wafanyakazi waliokuwa wakilipwa kwa zaidi ya miaka mitano hizo account namba zimepotelea wapi?
 2. Hakuna mfumo wa kutunza kumbukumbu katika halmashauri zetu?
 3. Wafanyakazi kuagizwa kila wakati kupeleka taarifa zao, hakuna system ya kutunza taarifa za wafanyakazi?, hakuna backup system ktk halimashauri zetu?

Mwezi uliopita(Oktoba) tatizo la kuchelewa kulipa mishahara lilijitokeza na nakumbuka ndg pinda alipoulizwa bungeni ktk kipindi cha maswali na majibu alisema kuna tatizo katika mfumo wa kumputer wa hazina wa kulipa mishahara na akaahidi kuwa halitajirudia tena!

Katika halmashauri kadhaa baadhi ya wafanyakazi hawajalipwa mishahara sijamsikia huyu ndg Pinda akiwaeleza Watanzania hawa wenye vimishahara kiduchu sababu ni nini? mfano katika halmashaur ya Meru ni wafanyakazi wachache waliopata mishahara!

Nimepata kusikia kuwa siku hizi mishahara inasubiliwa tra wakusanye kusanye then wanapeleka Hazina, kwenye tr 25 hivi then ndio Hazina wapeleke hazina ndogo kwa ajili ya malipo! sasa najiuliza kama maneno hayo ni kweli, inaweza kuwa mwezi huu hazikutosha? ndio maana wamelipwa wachache?

Naomba kuweka mjadala huu mezani na kama kuna anayeweza kuboresha zaidi ili tujue hatima ya nchi yetu bila kujali uchama wetu na isiasa wetu!

Naambatanisha majina ya baadhi ya waliokosa mishahara mpaka sasa pamoja na tangazo la moja ya halmashauri likiwaeliza wafanyakazi waliokosa mishahara!!!!!

Nawakilisha!
 
Attachments

 • IMG0087A.jpg
  IMG0087A.jpg
  223.9 KB · Views: 123
 • IMG0088A.jpg
  IMG0088A.jpg
  296.2 KB · Views: 117
 • IMG0089A.jpg
  IMG0089A.jpg
  262.4 KB · Views: 84

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,505
2,000
Litakuwa tatizo laki operations hili.

Nadhani Hazina wanahusika moja kwa moja.
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,088
2,000
Uwajibikaji ni function ya watawala. kama watawala ni mazezeta the output yaan utekelezaji wa majukumu na uwajikaji navyo

vitakuwa uzezeta. Hakuna wa kuwawajibisha zaid ya kuwa na waimba mashairi na ngojela majukwaani kwa kusimamia na kutetea

utekelezaji wa takwimu za kubumba, feki na za kipropaganda, wakiacha inchi ikiyumba na kuteketezwa. Hiyo ndiyo serikali ya ccm

chin ya Kikwete. (Nani anajali hali za wafanyakazi hawa na familia zao? who cares ??? no one the song in them is CHADEMA,

CHADEMA wakisahau hata majukumu na wajibu wao.)
 
mazegezege

Member
Mar 11, 2012
27
0
litakuwa tatizo laki operations hili.

Nadhani hazina wanahusika moja kwa moja.

kama kweli wanahusika hazina, mwezi wa kumi ilitokea na mkuu wa pm akaahidi haitajirudia tena, na sasa imerudia hatua zipi zimechukuliwa kwa huo uzembe? Watu wanalala njaa na kukopakopa na waliofanya uzembe wanaendelea kupeta duuuu!!!!
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,088
2,000
lakini mbunge wa meru ni cdm amesema lolote?

Mkono mtupu haulambwi, yeye hayuko hazina, aongee au aongee kwa maana ya kutoa pole? serikali iko wapi na inafanya nini?

mambo ya kupayuka kama akina Nape hatakama uwezo wa kutatua tatizo hawana ni bora kuwaachia Akina nape. mbuge hapaswi

kulipuka nakupayuka ovyo asikike kaongea hatakama hanalamsingi.
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Naona uzembe ni pande zote. Si waseme kuwa hawana pesa imeishia kwenye siasa chafu na kuzurura kwa rais wao. Shame on them all!
 
Kidatu

JF-Expert Member
Jun 11, 2008
1,508
1,250
Jamani hayo ni matatizo ya kiufundi tu na ni jambo ambalo linafanyiwa kazi. Serikali haiwezi kukosa mishahara ya kuwalipa watumishi wake.
 
Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Jamani hayo ni matatizo ya kiufundi tu na ni jambo ambalo linafanyiwa kazi. Serikali haiwezi kukosa mishahara ya kuwalipa watumishi wake.

Usiwatetee. Ni makusudi,

Hebu ona hili

There is a circular from Utumishi that all July 2012 promotion salaries > have been deferred until April 2013 and there shall be no arrears; and no > annual increment for 2012/13; no reasons were given for these decisions. > Interestingly, a letter from Hazina (a week earlier) had allocated funds > for both promotions and annual increment! > d. Treasury still remitting employers pension contribution instead of the > Universities (according to the SSRA and PPF acts)and which has brought a > lot of complexities
 
Kila serikali hapa duniani kwa sasa wanapunguza hayo mafao kwa wananchi wao, itakuwa Tanzania?.

Msipende kuilaumu serikali kwa kila jambo. Jaribuni kukaa chini na kuangalia ukweli halisi wa mambo.
 
OPTIMUS TZ

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
391
0
President Jakaya Mrisho Kikwete former government Master of Ceremonies ,
Chief political advisor Bi Salama Kitwete former standard 2 kiwahili teacher,
Chief political advisor Ridhiwani Kikwete

Hakuna rangi mtaacha ona kama hamridhiki mlishaelezwa mgogoro wa nini acheni kazi!
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,778
2,000
Tatizo dogo hilo mkuu,,we fika pale ministry of finance headquarters muone assistant commissioner of budget wagebill management and control anaitwa mr cheyo,,third floor room no 324 atakusaidia bila kinyongo,mlokole mmoja safi sana sijapata kuona,,

na kazisaidia halmashauri nyingi ..
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
1,500
Mnafikiri yale mapesa ya kugharamikia MKUTANO MKUU WA CCM KIZOTA yalitoka wapi, kama sio hazina.

FYI, hakuna matatizo ya ufundi wala nini, mwezi huu mishahrara italipwa 15/12. Mkutano MKUU WA CCM ulikausha HAZINA yote. Hiyo kwamba account number hazionekani, pelekeni particulars upya ni danganya toto ku-buy time wakati TRA wakiendelea kudunduliza.
 
Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Kila serikali hapa duniani kwa sasa wanapunguza hayo mafao kwa wananchi wao, itakuwa Tanzania?.

Msipende kuilaumu serikali kwa kila jambo. Jaribuni kukaa chini na kuangalia ukweli halisi wa mambo.

Ukweli upi? Be specific.
 
Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Mnafikiri yale mapesa ya kugharamikia MKUTANO MKUU WA CCM KIZOTA yalitoka wapi, kama sio hazina.

FYI, hakuna matatizo ya ufundi wala nini, mwezi huu mishahrara italipwa 15/12. Mkutano MKUU WA CCM ulikausha HAZINA yote. Hiyo kwamba account number hazionekani, pelekeni particulars upya ni danganya toto ku-buy time wakati TRA wakiendelea kudunduliza.

Na huenda ndo maana mafuta yakapanda!
 
sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,282
2,000
Jamani hayo ni matatizo ya kiufundi tu na ni jambo ambalo linafanyiwa kazi. Serikali haiwezi kukosa mishahara ya kuwalipa watumishi wake.

Kama ni makosa ya kiufundi, kwa nini siku hizi mishahara ianze kutoka tarehe 35 ya kila mwezi badala ya 25 ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom