Ni uzembe na ujinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni uzembe na ujinga

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mwiba, Oct 10, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Inaweza kuwa huna kitu lakini watu wakakuchukia na binadamu kumchukia binadamu mwenziwe ni kuwa na roho mbaya tena mbaya sana,huwezi kujua lakini jamaa alieondoa topiki ya ..Kesho ni mwisho wa dunia.. natangaza rasmi kuwa ana roho mbaya tena amejivalisha ngozi ya kondoo ,na kwa sababu yeyote ile aliyoiona yeye haswa kuondoa joke ile kwenye chumba cha jokes ni kuonyesha dhahiri ubaya wa roho yake ,hivi amewahi kusikia April Fool ,too much know without knowing ndivyo alivyo alieondoa mada.
  Hivyo ndugu nimekuweka katika kundi la watu wenye roho mbaya ,samahani lakini ndio hivyo ,ufahamu tu kuwa kwa upande wangu nakuona huna maana hata moja zaidi ya kupata kibarua cha kubabaisha na kujifanya unajua kila kitu ,na iwe hivyo lakini roho yako mbaya sana ,inawezekana wewe mwenyewe hujijui kama una roho mbaya na kujiona ni mchangamfu mjuaji na muekaji ukumbi huu sawa ,kwa mawazo yako yanapokupeleka unaona upo juu ya sheria na huwezi kuguswa na kitu chochote kile unavyojiona kuwa hata Mungu hawezi kukuingilia katika mambo yako ,ni uzubaifu wa kukosa la kufanya. Na ndio maana watu weusi hatufanikiwi wala hatuendelei kwa sababu hizo zilizokufanya kuona ile sio jokes hakuna tofauti na choyo cha mafisadi wanaohujumu uchumi wa nchi hii kwani wao roho zao hazina tofauti na yako ,na jichunguze utaliona hilo,analoandika John na Jacob na dada yao Marry hayo kwako ndio ya maana na unayoyashangilia na yanayofaa kuwepo hapa.
  Nafurahi kuwa hapa silipii kama ingekuwa nalipia basi timgetafutana ukanirudishia ela yangu.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhhh.kumekucha.
   
 3. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 779
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 80
  Mwiba si topic tu ya Kesho ni mwisho wa dunia iliyoondolewa zipo nyingine zilizopata dhoruba hiyo pia. Nashukuru umeliona hili, imagine ukiuliza unajibiwa 'sasa tufanyeje'. Nafikiri sisi ndiyo tunaifanya JF kwa kutumia hata muda kuandika, kusoma na kuchangia ni lazima tulitambue hilo.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo hawa wajamaa wanajiona ni wao tu yaani wanavyojiona ni sawa na inavyojiona CCM hapa Tanzania ,lakini wanasahau tu ngoma ikivuma sana ujue mwisho wake itapasuka tu na kama unavyoiona CCM imejaa nyufa zinazoashiria ndio mwanzo wa kupasuka basi na hawa naona wapo njiani ,kama utakumbuka ilikuwepo Jambofurums jinsi ilivyokuwa ikivuma tulisema sasa mambo mazuri na Mtz amepata pa kujifaragua kufumba na kufumbua haijulikani hata ilipokufia ,katika kujikurupusha na kuonyesha kuwa mambo shwari wakavumbua kuwa wamebadilisha jina na sasa ni jamiiforums ila wamesahau kitu kimoja kumalizia Ujamaa na kujitegemea.
  Yaani hata wakiulizwa kwa nini wameondoa ile jokes katika sehemu yake nakuhakikishia watakuja na jawabu utumbo mtupu,hilo halina upinzani kabsaa ,ila sishangai sana maana ndio kazi yao inayowapatia tonge.
   
 5. m

  mcferry Member

  #5
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lets grow up guys and have freedom of expression,any body can write anything as long as is not personal attack or fear of causing unrest in the jamii.
  hakuna haja ya kuondoa mada ya mtu mwingine kama haina madhara yeyote jamani
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pole mkuu, JF ndivyo ilivyo....!
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mi nilishanyofolewa topic zangu humu na ukiuliza unaonekana **** tu. Hakuna anaejibu. Ukiropoka ndo 'unajibiwa'
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nimefuatilia kwa karibu ,kumbe nimeambiwa ukionekana hapa ni mkandiaji wa CCM siku hizi tumazokaribia uchaguzi basi utakachoandika kinaondolewa na wameambiwa wasichague ni wapi au topiki gani ,amri waliyopewa ni kuiondoa topik ya wapinzani wa Chama Tawala.

  Kama ukiangalia kule kwenye jukwaa la siasa topiki karibia zote ni za CCM iwe inaponda au inaunga mkono mradi iwe ni ya CCM ,na elekeeni kule kwenye jukwaa la siasa, muone hakuna Chadema wala CUF ni CCM na kama utaiona basi hiyo ilikuwa kabla ya amri kutolewa toka kwa wakubwa zao. Inawezekana kabisa wakajitetea lakini ukweli wamepewa amri ,haina haja ya kusema nani katoa amri maana hali yenyewe haihitaji mwenye macho hata kipofu akipapasa kwa kuuliza ili asomewe yanayojiri ataambiwa hapana topiki inayohusiana na harakati za vyama vya upinzani zote zinaihusu CCM.
  Nawapa pole sana.
   
 9. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Makubwa!!!!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hizi tuhuma ni nzito naomba wahusika wazijibu..
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mi niliiona thread hiyo jana na nikaichangia sawia...Lakini leo naitafuta nione michango ya wengine nastuka haipo tena.
  Basi hawa jamaa zangu wangekuwa wanamPM mtu aliyeipost kumjulisha kilichojiri, kuliko kukaa kimya na kusababisha watu waje hapa na hasira zao kuuliza kulikoni!
  Mods tupeni majibu stahiki ya tuhuma hizi.
  Lakini pia ni kweli kwamba mmekuwa tawi la CCM siku hizi?
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yaani hata ukimuona Tembo na wewe upo mbugani utahitajia mabwana pori wakupe jawabu kuwa ni tembo ? Naona watakwambia ni kifaru tu .ili kukuwacha kwenye mataa. Na hii kazia haiwezi kujibika kama hawajakuja na ushahidi wa kina kuhusiana na ile mada ...Kesho ni Mwisho wa Dunia...! Mwana Jf utafanya nini ? Yaani mistari miwili hiyo tu ,wamekuja na paranja wameondoa na kuweika kwenye ushahidi kuwa ikiwa patahitajika sababu ya kuonyesha waonyeshe sababu kutokana na mistari iliyopo kwenye hiyo mada husika ,lakini hapa naona wamejikojolea inabidi kindumbwendumbe ,ni mambo ya kuchamba kwingi waliyonayo !!

  Mada nimeiburusa kutoka kwenye forum za kizungu na huko imejaa replies kibao si moja wala mbili ni kama page sita na watu wanainjoy namna watakavyofanya na kujiandaa ikiwa siku hiyo itatangazwa & alot of jokes inside that topic.

  Ila hapa pangu pakavu wameiona ni ya mpinzani ndio wakapata kibarua cha kuiondoa.

  Kama haitoshi kule kwenye chumba cha ngono ambako ndiko kwenye aibu ya Jamiiforums, kuna topiki hazina muelekeo wa jamii ni sawa na site za porno ambazo hazilingani na hapa kwa nionavyo, basi hata ukiwaunga mkono katika kuendeleza mambo yao basi kwa kuwa unanuka upinzani wataondoa na kukukejeli kuwa umeleta mada iliyovuka mipaka ,wakati kuna mada ni aibu tupu ,wao wanaona wengine tukishiriki kule ndio mambo tunapenda au tunaona yanafaida na kufaa ,wanashindwa kuelewa kuwa katika kiswahili kuna msemo usemao ukienda sehemu na ukiona watu wote wanachongo na wewe ziba lako jicho moja.

  Ila hapa hata ukiziba jicho watakuona wewe ni chongo zaidi ,na umewazidi katika uchongo wao.
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,763
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tuhuma hizi ni kubwa kweli tafadhali jibuni tena bila unafiki wowote!
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mwenzenu anakula ban....hahahahaha!
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Heeeeeeeee kumbe imekuwa hivi...........kazi basi.....duh
   
 16. GP

  GP JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  duh, sio mchezo sijui miezi mingapi

  Mwiba
  Mwiba has no status.
  Banned
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahaha!dude vipi,upo masaki?
  kama vipi twende zetu........
   
 18. Bang'a

  Bang'a Member

  #18
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polen CCM, lakn hatutaacha kuwaandika kwa maufisad myafanyayo. Na kwa taarfa yenu mtapakwa had mtafunga JF. Futen topic zote, ila hamtafuta yaliyo ubongon mwetu. Shame on u!
   
 19. Bang'a

  Bang'a Member

  #19
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tetes mnataka kununua JF, na vikao vya manunuz 2meshasikia gosping zake, ngoja 2shke mafail tutaqoute mpaka finger prnt. Wana JF kaen mkao wa kurusha mawe kwa wenye nyumba za vioo!!!
   
 20. M

  Mende dume Member

  #20
  Nov 5, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF

  I greet you in the name of whatever Gods you believe and in the name of my official philosopher, the person who loved Tanzania more than Tanzania loved him.

  this is none other than.... JK Nyerere, the true son of Africa.

  nawasilisha

  Mende dume (haitishwi na Harufu)

  NB- wana JF nimeona post zinazomfananisha JK nyerere na JK mwingine- sio sasa mimi naona maana yule sio JK ni JM. remember K is for Knowledge but M? who knows am sure Maarifa is not part of it.
   
Loading...