Ni uzembe kuendelea kuipamba Dar kwa flyovers wakati shuleni na hospitalini hakuna nyumba na vifaa vya kutosha

Nimeona clip ya Polepole akimsifu Magufuli wakati akisoma kitabu ambacho nadhani ni ilani ya chama. Anachokitaja ni idadi ya flyovers zinazopangwa kujengwa; Moroko, Tazara, Magomeni, Mwenge, Chang’ombe na uhasibu, fire, Kinondoni, etc. Huu ni uhuni na ushenzi wa matumizi ya pesa ya taifa hili. Ni uhuni kwa sababu. Pesa ya nchi isigeuzwe kuwa ni pesa ya kuipamba Dar es Salaam kwa sababu za kisiasa. Nchi hii bado sana! Tuna mahitaji kibao.

Kinachosikitisha ni mahitaji mengi tuliyonayo kwenye mambo ya msingi. Shule zetu bado zinaonekana kama mabanda ya wakimbizi. Shule hazina nyumba za waalimu, hakuna maabara, hazina waalimu, hazina vifaa vya sayansi na matokeo yake watoto wote wa shule za vijijini hakuna anayesoma sayansi. Wanasoma masomo wanayoyaita ya arts wakati Kiingereza hawajui kabisa! Hospitali wanazojenga hazina vifaa, nyumba za watumishi hakuna! Sifa za aina hii ni upuuzi mkubwa sana!

Anayewaandikia hizo ilani ana matatizo na hii ndo mbunge mmoja wa CCM aliwahi kuwaita vijana wa Oysterbay! Hawa wanadhani TZ ni Dar tu! Itakuwa bahati mbaya sana kama kweli awamu ijayo itakuwa ni ya kujenga flyover Dar, barabara Dodoma na kuamini ndo maendeleo. Nchi hii ni kubwa.
Uwa naamini kuwa Elimu yetu inadidimia chini kwa kukosa maarifa.
Umenena vyema.
 
Nataka tanzania iwe kama Uraya, nataka wazungu watoke uraya waje watibiwe tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uifahamu nchi yako vizuri na maendeleo yake, na hii inaonyesha ni kiasi gani hamna mipango madhubuti kama wapinzani mmejazwa maneno ya kuambiwa vichwani mwenu na kukaririshwa kwamba hakuna jema linalotendwa na serikali

Na hii ni mbaya zaidi kwa sababu inaonyesha jinsi gani vichwa nyenu havina uwezo mzuri wa kuchambua mambo na kubaki kulishwa na kuaminishwa mambo na mnayapokea kama yalivyo pasipo kuyafikiria. Poleni na tambueni hii ni Tanzania ya Watanzania kwa ajili ya Watanzania.
Yaani Kama wewe ndo una akili,halafu unapost hvi??
 
Back
Top Bottom