Elections 2015 Ni uvumilivu wa Wapinzani unayoiponya Tanzania

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Kuna watu wana tabia ya kupinga kila kitu hata kama ukweli unaonekana wazi watapinga tu.

Mimi naamini hiki ninachokiongea ni ukweli usiopingika, uvumilivu wa wapinzani ndio umeiponya tanzania kutokuwa na machafuko hadi sasa, maana serikali ya CCM mara kwa mara wamekuwa wakifanya mambo mengi ambayo yangesababisha nchi kuingia kwenye machafuko makubwa kama si uvumilivu wa wapinzani.

Kwa bahati mbaya wanadhani kwamba kwa kuwa wanamiliki vyombo vya dola basi wanahaki ya kunyan'ganya haki za watu wengine wamesahau kwamba mwanadamu ni mwanadamu tu, hivyo vyombo vya dola wanavyojivunia siku moja.

Vitawachoka kwa makusudi tumeona kila mahali wapinzani waliposhinda wamefanya hila eidha kunyan'ganya haki au kutaka kunyan'ganya. Mfano mzuri ni Tanga, kilombero, Dar es salaam na maeneo mbalimbali nchini kama siyo uvumilivu wa wapinzani nchi ingekuwa imeingia kwenye machafuko.

Zanzibar CCM ilishindwa ila wanalazimisha tu na hao viongozi wanaojiita wapenda amani wamenyamaza wakati haki inaporwa.

CCMwamekuwa wakitumia propaganda mbaya kwamba CUF ikishinda wakristo watafukuzwa Zanzibar, mimi ni mkristo siamini huo uchanganishi ukristo upo saudia,iraq na nchi ambazo zina utawala wa kiislamu.

CCM mtakuja kujutia siku moja acheni kuchezea amani.
 
Mnapogombea lengo ni kushika dola hizi kauli za kuiponya nchi ni ya kipuuzi 100% kwani kwa nini mwenzako hawazi kuponya nchi? Kauli za kinafki hizi ngoja watawale karne nyingi alafu nyie muendelee kuiponya nchi. Hatuwataki wagombea wa namna hii kama haki haitendeki react kutafuta kwa nguvu. For others to survive others must die.
 
Back
Top Bottom