Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
Baba ni baba, haitatokea masikio yakazidi kichwa,na yakizidi hukatwa haraka ili yasiwe kama ya mnyama sungura.
Unapomkosoa vibaya baba yako, hakupi alichotegemea kukupa, hachukui mawazo yako mazuri, anakupotezea katu. Atakuwa anakuangalia tu. Penseli yako ikiisha shule anakuangalia tu, badala ya kukupa nyama sasa anakupa makande,ni kwa sababu ya utukutu wako. Kiatu utakivaa mpk soli itoboke, hali kadhalika kaptula yako itaota viraka,akikuangalia tu. Atakuwa anadeal na watoto wasikivu, watiifu na wanaomsikiliza.
Viongozi wa nchi wanapambana kuweka mambo sawa,mambo yaliyoenda mrama na sote tunajua. Tuwage na kumbukumbu basi.
Kuna watu wanawasema vibaya viongozi wetu,ili iwe nini? Na ukishakashifu,nini kinafuata sasa? Ndo atakupa maziwa na asali? Subutu yako. Wewe ni wa kupewa pilipili kichaa ili utafune debe zima.
Kuna watu hawaoni jema. Kila kitu kibaya, kila kitu hakifai. Huu ni utovu wa nidhamu na ni ukosefu wa adabu, hata Kama wewe ni mtu mzima.