Ni utaratibu upi wa kufuata ili kuvuta umeme (TANESCO) kwenye nyumba

mzizi1

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
255
692
Mimi nipo huku mkoani kwa sasa, nahitaji kuvuta umeme kwenye nyumba ya mzee huko Mwanza (Ilemela) lakini nimepata mkanganyiko kidogo.

Kwa taarifa alizonipa ni kuwa, kuvuta umeme ni laki tatu na 20 (320,000)

Eneo tulilopo kuna nguzo tayari na hata mita 20 hazifiki. Maana yake ni kuwa wao (TANESCO) itahitajika waweke mita pekee, nishafanya wiring na kila kitu kinachohitajika.

Hii bei (320000) kwakweli imenivunja moyo kabisa wa kukamilisha hili lengo.

Naombeni Mwenye msaada kuhusu hili na maoni basi anisaidie kuniongezea uelewa, naona ghalama ni kubwa sana.

Nawasilisha
 
Ni laki na sabini na saba kuvuta umeme in means hiyo ni ya mita ndio iko hivyo
 
No laki na sabini na saba kuvuta umem in means hiyo ni ya mita ndio iko hvy
Sio kweli kwa kiasi hicho ulichosema!!kiasi hicho ni kwa maeneo ya vijijini tu, ila kwa maeneo ya mjini, (miji, majiji) kuunganisha umeme bila nguzo ni 320, 000(kama upo ndani ya mita 30 toka ilipo nguzo)
 
Ingekuwa lakitatu kama unanua nguzo na kuwek umem.lakin kwakua unanguzo jiran haifki hiko kias maan 177000 mita na sijajua iko veep?
Hiyo bei ni kwa maeneo ya vijijini!!kwa mijini hiyo aliyoambiwa ndio bei halisi.na yeye ilemela ni mjini
 
Pole sana kaka, vema umeshirikisha richa ya kuvunjika moyo.

Mkuu kwanza TANESCO wana bei mbili,

1- kwanza ni ya kawaida ambayo hulipwa na waishio mijini (utambuzi wa maeneo wanao tanesco)

Hii Ina kuwa 321,000 ikiwa ni gharama ya meter tu.
Ikumbukwe kuwa, nguzo za TANESCO haziuzwi hata mia ila kwa kutojua wengi wameuziwa hati 500,000 kwa nguzo.
Ukiona afisa anakupa bei ya nguzo weka mtego fasta.

2-Tanesco wana idara yao inayo fanya kazi chini ya REA .
Hii hufanya kazi maeneo yote ya mashambani/vijijini.
Bei za chini ya REA ni 27,000 tu kwa meter.

177,000 ni makadirio wanayo fanya kwa installation ya mfumo wa umeme kwa kila kitu hadi angalau taa moja iwake.

Hitimisho.
Bei ulo ambiwa kwa ilemela ni sawa 100%

Asnte
 
Safi kabisa.

Picha ya pili namba TANESCO TAIFA.
Picha ya tatu,namba TANESCO Mkoa wako wa mwanza.
Make call.

Au nenda jamii forums}Hoja mchanganyiko} TANESCO special tread, halfu eleza utajibiwa hapo hapo
Screenshot_20210115-133103.jpg
Screenshot_20210115-133214.jpg
Screenshot_20210115-133146.jpg

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • Screenshot_20210115-133146.jpg
    Screenshot_20210115-133146.jpg
    40 KB · Views: 7
Mimi nipo huku mkoani kwa sasa, nahitaji kuvuta umeme kwenye nyumba ya mzee huko Mwanza (Ilemela) lakini nimepata mkanganyiko kidogo.

Kwa taarifa alizonipa ni kuwa, kuvuta umeme ni laki tatu na 20 (320,000),
Eneo tulilopo kuna nguzo tayari na hata mita 20 hazifiki. Maana yake ni kuwa wao (TANESCO) itahitajika waweke mita pekee, nishafanya wiring na kila kitu kinachohitajika.

Hii bei (320000) kwakweli imenivunja moyo kabisa wa kukamilisha hili lengo.
Naombeni Mwenye msaada kuhusu hili na maoni basi anisaidie kuniongezea uelewa, naona ghalama ni kubwa sana.

Nawasilisha
Tafadhali fika ofisini na kitambulisho tukuhudumie gharama zote zinatolewa kwa maandishi hivyo tusikiloze sisi kwa huduma bora
 
Pole sana kaka, vema umeshirikisha richa ya kuvunjika moyo.

Mkuu kwanza TANESCO wana bei mbili,

1- kwanza ni ya kawaida ambayo hulipwa na waishio mijini (utambuzi wa maeneo wanao tanesco)

Hii Ina kuwa 321,000 ikiwa ni gharama ya meter tu.
Ikumbukwe kuwa, nguzo za TANESCO haziuzwi hata mia ila kwa kutojua wengi wameuziwa hati 500,000 kwa nguzo.
Ukiona afisa anakupa bei ya nguzo weka mtego fasta.

2-Tanesco wana idara yao inayo fanya kazi chini ya REA .
Hii hufanya kazi maeneo yote ya mashambani/vijijini.
Bei za chini ya REA ni 27,000 tu kwa meter.

177,000 ni makadirio wanayo fanya kwa installation ya mfumo wa umeme kwa kila kitu hadi angalau taa moja iwake.

Hitimisho.
Bei ulo ambiwa kwa ilemela ni sawa 100%

Asnte
Hapa kwenye nguzo hapa ni kizungumkuti....hivi huyo Ofisa anapata wapi 'guts' za kumwambia Mteja alipie nguzo? tuanzie hapo kwanza.

Kuna Mkanganyo mahali.
 
Back
Top Bottom