Ni utaratibu gani wa kufanya nikitaka kubadili jina kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni utaratibu gani wa kufanya nikitaka kubadili jina kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Isimilo, Sep 14, 2010.

 1. Isimilo

  Isimilo JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau
  naomba kujua kama is possible kubadili jina ili hali document zangu kama certificates na passport ziko kwenye jina lingine. nataka kubadilisha first name na kutumia jina la ukoo kama Surname badala ya jina la Baba ambalo ni 'common name'. na- feel kama sionyeshi uasilia wangu kwenye majina yote mawili kwa kuwa yote ni ya kisasa. je inawezekana kuomba ceertificate zangu za elimu ya juu zingine zinazofuata pia ziwe ktk jina jipya ingawa kwa sasa natambulika kwa jina hili kitaaluma?

  thanks
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Inawezekana..........lakini hiyo reason ya kutumia surname ili kuonyesha uhalisia kwenye vyeti, naona ni week reason. Kama una birth certificate yenye jina la ukoo then you should have passport yenye jina lako, la kati na jina la ukoo....then thats it. uhitaji documents nyingine ziwe ka jina la ukoo.
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280

  ukitaka kubadili jina ni rahisi ingawa ni hatua kidogo.Unajaza document inayoitwa deed poll,ambayo inashuhudiwa na Wakili.Baada ya hapo unapeleka kwa msajili wa nyaraka pale wizara ya ardhi kwa ajili ya usajili ukiambatanisha na ada kidogo.Deed poll ikishasajiliwa,unapeleka nakala moja kwenye ofisi ya mchapa magazeti wa serikali tayari kwa ajili ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali.Hatua hizi zaweza kukugharimu si chini ya miezi miwili.
   
 4. m

  mtakatifutz New Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani na mimi ninashida hiyo naomba msaada, ni kijana mwenye 31 yrs, nililelewa na baba wa kambo mama aliniandikisha kwa jina la baba wa kambo kwenye birth certificate, sasa nimekuwa yule baba alifariki na mama pia so najiona sibelong kabisa huko kwa baba wa kambo kwani wananitenga na mama yangu walikuwa hawampendi, kwa baba yangu mzazi(ambaye pia amefariki) hawana shida kabisa, nilioa kwa jina la baba mzazi na watoto wangu wanatumia jina la ukoo wa baba yangu mzazi kwani mke wangu alikataa katakata kutumia jina la baba wa kambo, sasa passport na vyeti vyangu vyote kasoro cha ndoa ni jina la baba wa kambo nifanyeje nibadili jina kwani naona vibaya wanangu kutumia jina tofauti na mimi.
   
Loading...