Ni utaratibu gani wa kisheria na kikatiba tunatakiwa tuufuatee kumuondoa raisi madarakani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni utaratibu gani wa kisheria na kikatiba tunatakiwa tuufuatee kumuondoa raisi madarakani?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Salary Slip, Sep 7, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,975
  Likes Received: 37,567
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu wenye kupende maendeleo ya nchi yetu naomba mtujuze ni utaratibu gani halali unatakiwa kutumika kikatiba na kisheria kumuondoa raisi madarakani.Sisi ndio waajiri wake ila ikifika hatua baadhi yetu haturidhiki na utendaji wake tunatakiwa tutafute njia halali za kisheria kumuondoa kwenye nafasi yake badala ya kila siku kuwa walalamikaji tu bila kuchukua hatua.

  Mimi huwa najiuliza hivi inakuwaje karibu nchi nzima kuanzia wanaharakati,wanasiasa,waandishi wa habari,makundi mbali mbali ya kijamii na watanzania wengi wakilalamika kutaka watu fulani, ambao wengi wao huwa ni wateule wa raisi, wachukuliwe hatua halafu hakuna kinachofanyika.Na hata pale hatua zinapochukuliwa basi huwa ni baada ya watu kulalamika na kupaza sauti sana.Sasa huyu mheshimiwa yeye huwa dhamira yake haimsukumi kuchukua hatua au yeye huwa haoni uchungu kama watanzania wengine?Uzalendo wa viongozi wetu uko wapi siku hizi?

  Ni jambo la kushangaza na kuhuzunisha kuona mpaka sasa IGP,na RPC wa Iringa bado wapo ofisini.Hawa ni watu ambao wakati uchunguzi unaendelea walipaswa kuwa teyari wameshajiuzulu au kuondolewa ktk nafasi zao.Hivi ule ushahidi wa picha hautoshi kuthibitisha ushiriki wa polisi katika unyama ule?Sasa hawa wakuu wao wa kazi mbona mpaka leo wapo ofisini na ukizingatia hizi tuhuma za polisi kuua raia ni jambo la mara kwa mara.

  Hali hiyo ya kulindana ilikuwa hivyo hivyo baada ya taarifa ya CAG kuonyesha uozo serikalini.Ilibidi kelele zipigwe ndio hatua zikachukuliwa.Sasa kwa mwendo huu tutafika salama hiyo 2015?Tuna haja kweli ya kusubiri mpaka muda huo ufike?

  Hivi leo hii nani anajua nini kinaendelea kuhusu Jairo,watuhumiwa wa richmond,kagoda,meremeta na wengine wengi tu.

  Swali langu ni kwanini sisi tuwe watu wa kulalamika tu bila ya kuchukua hatua za kinidhamu kama ambavyo yeye hutishia kuwachukuli hatua walimu na madaktari waliogoma?Yeye kama mtumishi wa umma si anapaswa kuwajibika kama watumishi wengine?

  Wanasheria aanzisheni mchakato wa kikatiba na kisheria na sisi tutawaunga mkono.Tusisubiri bunge limuwajibishe kwani lile bunge liko kichama zaidi.Vinginevyo tutendelea kulalamika mpaka 2015.

  Nawasilisha.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ni wazi kwamba kama itafikia hatua ya Rais kuondolewa kisheria wewe hutahusika na kwa maana hiyo huna sababu ya kutaka kujua, wewe unaonekana kushiba chai ya asubuhi na kuanza kubwabwaja. watu kama wewe hawana nafasi yoyote ya kujua sababu za kumuondoa rais madarakani. Hata kama ni waasi, wewe huna chako bali utakuwa unafuata mkumbo tu. Nenda chooni kanye subiri chakula cha mchana kula kulala wewe.
   
 3. k

  kiwososa JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,083
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hatuitaji matusi humu toa hoja kama alivyotoa mwenzio kama huwezi timua mbio. KILAZA WEWE. NJAA ZAKO ZITAKUUA
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,975
  Likes Received: 37,567
  Trophy Points: 280
  Hivi kila mtu akiamua kutukana na kutumia lugha kama yako hii jukwaa litakuwa na maana kweli!

  Nani asiyejua kutukana!

  Nikikujibu kwa matusi itanisaidia nini?

  Hapa mtu akileta hoja jibu hoja

  Hata huyo unae mtetea unamtia fedheha tu.

  Ama kweli kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo.
   
 5. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red panakuhusu wewe
   
 6. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kabla hujapewa taratibu hzo za kisheria na kikatiba tupe sababu za kisheria na kikatiba zinazo kusukuma kutaka kumuondoa raisi madarakani kwasababu unao wataja Wanaharakati=WAPIGAKERERE
  Wanasiasa=MAFISADI na WAROHO
  Waandishishi= WATUMIWAJI
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,975
  Likes Received: 37,567
  Trophy Points: 280
  Unauliza sababu!

  Inawazekana unaishi ughaibuni.
   
 8. C

  Cartoons Senior Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wewe kama raia huna nafasi ya moja kwa moja,ila waweza kufanya hivyo kupitia kwa mbunge wake,ambaye atatakiwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi.
   
Loading...