Ni utajiri gani wa kukomba pesa za NSSF na PSSF halafu unaita hii nchi Tajiri? Wastaafu hawajalipwa wamegeuka tegemezi

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
171
1,000
Hili ni swali baada ya uchumi wetu kuporomoka mpaka kufika asilimia 4.8%.Wakati huo takwimu zilifichwa na kutungiwa sheria kali sana. Television ya Taifa ( TBC) iliongoza mapambio ya kusifu kwa Ngonjera, ngoma na vinanda kuwa mambo ni mazuri

Wazee wastaafu wanafuatilia mafao yao huko NSSF na PSSF zaidi ya miaka miwili bila mafanikio, Omba sana hali ya Uzee isikukute Jitahidi kurudisha umri nyuma usipende kusherekea mwaka mpya, labda sema na kuimba "Forever Young" yaani "ujana daima"

Mapambio na Ngonjera yaliaminisha ni pesa za ndani kumbe ni pesa za wastaafu na wazee na mingine ni mikopo isiyokuwa na kichwa wala miguu ambayo takwimu zake zilifichwa huku TBC Taifa ikiimba wimbo wa beberu mbaya mchana mbele ya Raia, Gizani waliimba beberu tusaidie tutakulipa taratibu

Je, kukwapua pesa za NSSF na PSSF ndio utajiri wenyewe?

Je, kukopa kwa siri ndio utajiri wenyewe?

Poleni sana wastaafu na ambao mnakaribia kustaafu karibuni hakika maisha yenu yanasikitisha sana

Kwa wale wenye wazee ambao wanafuatilia pension miaka Nenda rudi jiandaeni kisaikolojia hakuna "Forever Young" Kuna muda mwili utakataa tu kufanya kazi

Nasikia kuna ahadi ya malipo na watu kuanza kulipwa wataanza wa mwisho kustaafu au wataanza wa mwanzo.

Je, itatumika nyuma geuka yaani wa mwisho atakuwa wa kwanza na wa kwanza atakuwa wa mwisho?
 

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
559
1,000
Jamaa alituangusha sana. Kuna wazee miaka mitatu hawajalipwa mafao yao.

Kitakachotokea kwa mama ni kubinafsisha rasilimali fulani kwa mabeberu mana serikali haiwezi kulipa madeni ya ndani, madeni ya nje, hapo hapo itoe ajira, hapo hapo ipunguze kodi.

Jiwe aliweza kubana kwa kuwa alikuwa ana roho ngumu
 

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,114
2,000
Ki ukweli mama anajitahidi sana na swala la uwazi ndo maana alianza na kuachia vyombo vya habari uhuru wake. Hapendi sifa zakijinga ambazo anaona hazistahili.

Magu ilikuwa ili uelewana nae basi upindiashe ukweli hapo ndo utakuwa rafiki yake na tena veo utapata. Akiona una sema ukweli tambua ushakuwa adui yake na utatafutiwa figusu kama akina Assad.

( Sio kwamba hakupambania nchi ila alipenda tudanganya na alitaki tuamini hilo hata kama tunaona ni uwongo) Achilia mbali tuu kusema fedha za ndani ila deni lataifa lilikuwa linapaa huko nje (Yaani kukopa kimya kimya).

Sa hivi anamtesa huyu mama mambo mengine haezi yasema japo twaona uwongo ulivyokuwa mwingi.
 

mtumishiwaleo

JF-Expert Member
May 4, 2020
419
500
Tatizo hili la mifuko ya pesheni halijaanza wakati wa Jpm,lilianzia kwa Mkapa walichukua wakajenga chuo cha Dodoma, Wakati wa Kikwete wakajenga daraja la Kigamboni na Mradi wa kujenga nji mpya wa Kigamboni.

Magufuruli kakuta mifuko ilisha filisika kitambo,sema kwasababu mlikuwa ampendi ndio maana mnamuangushia jumba bovu.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,303
2,000
Hasa wale waliokua wafanyakazi iliyokua EAC hadi leo wengi wao wametangulia mbele ya haki bila ya kulipwa mafao yao na tuelewe malipo haya fedha yake haikua ya serikali
 

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
3,671
2,000
Ivi wale SSRA wana jukumu gani sasa iv maana wapo kimyaaaaaa kama maji ya mtungi . Naona ni kheri raisi akaivunja hii taasisi
 

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
13,087
2,000
Tatizo hili la mifuko ya pesheni halijaanza wakati wa Jpm,lilianzia kwa Mkapa walichukua wakajenga chuo cha Dodoma, Wakati wa Kikwete wakajenga daraja la Kigamboni,na Mradi wa kujenga nji mpya wa Kigamboni.Magufuruli kakuta mifuko ilisha filisika kitambo,sema kwasababu mlikuwa ampendi ndio maana mnamuangushia jumba bovu.
Kipindi kipi wastaafu walitekesa kufuatilia mafao yao?
 

Fernando Jr

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
2,450
2,000
Binafsi nilikuwa nikisikia mtu anasema/anaamini serikali 'ya magufuli' ina hela au kuiamini kwa jambo jingine lolote hasa kwenye takwimu nilimwona mjinga sana. Uminyaji wa uhuru wa habari ni kiashiria cha mwanzo kabisa cha utawala wenye mashaka, na utawala wenye mashaka hautakiwi kuaminiwa kwasababu tayari ni wa mashaka, kila jambo litakuwa kimashakamashaka.

Kuna watu wangu wa karibu waliokuwa wakiniona hater nikikosoa upuuzi (nimetumwa na mabeberu). Leo yote yanayofichuliwa sishangai kwasababu nilijua ndiyo yaliyokuwa yakiendelea. Lakini sasa wao ndio wananifuata na kusema 'aisee kumbe ulikuwa sahihi!' nami huwajibu 'tulieni mtajua uozo mwingi tu'.
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,092
2,000
Baada ya kuiba pesa za wanachama wakaja na mpango wa kuiunganisha hii mifuko, kufukuza watu Kazi Ili kuwazulumu michango yao,mambo ya kikokotoo wizi mtupu,fao la kujitoa ukae miaka 50 ndo upewe chako uliona wapi hii duniani hii utadhani una garantii na Muumba hii ni dhuluma.Wezi wengine wakazawadia ubalozi Ili wakazitumbue zaidi badala ya kuwa unasema vipi una pesa hali uzalishaji export imekufa.
 

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,097
2,000
Tatizo hili la mifuko ya pesheni halijaanza wakati wa Jpm,lilianzia kwa Mkapa walichukua wakajenga chuo cha Dodoma, Wakati wa Kikwete wakajenga daraja la Kigamboni,na Mradi wa kujenga nji mpya wa Kigamboni.Magufuruli kakuta mifuko ilisha filisika kitambo,sema kwasababu mlikuwa ampendi ndio maana mnamuangushia jumba bovu.
Muongo . Udom imejengwa na kikwete
 

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
1,066
2,000
Baada ya kuiba pesa za wanachama wakaja na mpango wa kuiunganisha hii mifuko, kufukuza watu Kazi Ili kuwazulumu michango yao,fao la kujitoa ukae miaka 50 ndo upewe chako uliona wapi hii duniani hii utadhani una garantii na Muumba hii ni dhuluma.Wezi wengine wakazawadia ubalozi Ili wakazitumbue zaidi badala ya kuwa jela.
Jamaa alikuwa tapeli sana
 

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
1,066
2,000
Ungelisema Magufuri alipora kiasi gani nalini,sio kuongea tu kutumia nimekwambi chanzo cha mifuko ya pesheni kuyumba toka enzi hizo za Mkapa, Alafu viongozi wa hiyo mifuko walikuwa wanajenga Majengo kwa garama kubwa,mpaka leo yamekosa wanunuzi,tenda mtoni kijichi,bunju,mabwe pande, Majengo yao yote yamekosa wanunuzi, kwasababu ya garama kubwa, Mifuko hii imefirisika kwasababu viongozi wao hawakuwa na maono na ufisadi, ndipo maana Magufuri alikwisha washauli kuwa bora wawekeze kwenye secta ya Viwanda kuliko kukimbilia kwenye kujenga majumba.
Pesa amejengea reli ya kuwalisha wazee angetoa wapi
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,768
2,000
Tatizo hili la mifuko ya pesheni halijaanza wakati wa Jpm,lilianzia kwa Mkapa walichukua wakajenga chuo cha Dodoma, Wakati wa Kikwete wakajenga daraja la Kigamboni,na Mradi wa kujenga nji mpya wa Kigamboni.Magufuruli kakuta mifuko ilisha filisika kitambo,sema kwasababu mlikuwa ampendi ndio maana mnamuangushia jumba bovu.
Ni swala la kikokotoo
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,540
2,000
Ungelisema Magufuri alipora kiasi gani nalini,sio kuongea tu kutumia nimekwambi chanzo cha mifuko ya pesheni kuyumba toka enzi hizo za Mkapa, Alafu viongozi wa hiyo mifuko walikuwa wanajenga Majengo kwa garama kubwa,mpaka leo yamekosa wanunuzi,tenda mtoni kijichi,bunju,mabwe pande, Majengo yao yote yamekosa wanunuzi, kwasababu ya garama kubwa, Mifuko hii imefirisika kwasababu viongozi wao hawakuwa na maono na ufisadi, ndipo maana Magufuri alikwisha washauli kuwa bora wawekeze kwenye secta ya Viwanda kuliko kukimbilia kwenye kujenga majumba.

Kwani uwanja wa ndege wa Chato unatua ndege ngapi kwa siku, ili tuone akili yake aliyowashauri hiyo mifuko ya jamii iwekeze kwenye viwanda? Lengo ni kuona faida ya huo uwanja wa ndege wa 39b, ili tupime akili yake dhidi ya ujinga wa hao watu wa mifuko ya jamii waliowekeza kwenye majengo hapa mjini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom