Ni utabiri wa Lowassa au Rostam?

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
883
Pengine post hii itahamishwa,hilo nawaachia wenye maamuzi ya kufanya hivyo.Nimekutana na hii "habari" (japo kimsingi ni makala ) katika gazeti la Rai toleo la wiki hii.Japo sio wazo la busara kuweka post hapa kwa kuongozwa na hisia,lakini nashawishika kuamini kuwa ujumbe uliomo kwenye makala hiyo unaweza kuwa wa EL au RA.Ni kama warning kwa CCM japo pia ni kama utabiri wa namna flani ambao inawezekana una ukweli ndani yake.All in all,ni jitihada za mafisadi kuhalalisha madhambi yao na wakati huohuo kutafuta sympathy ya chama kwa kigezo cah kuiimarisha CCM

Makala nayozungumiza ni hii hapa (japo inapatikana pia kwenye link hapo juu)

`CCM yagawanyika`

:: Makundi yatishia uhai wake

na mwandishi wetu

YAPO mawazo miongoni mwa jamii kwamba yaliyotokea katika mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika Dodoma hivi karibuni, ndiyo unaweza kuwa mwanzo wa kumomonyoka kwa Chama Cha Mapinduzi.

Mawazo hayo, yanatokana na ukweli kwamba yaliyotokea Dodoma, yanavinufaisha vyama vya upinzani ambavyo kwa muda wa miaka 16 vimekuwa vikitafuta mwanya bila mafanikio na kwamba nafasi hiyo imepatikana kwa CCM kuamua kujidhoofisha chenyewe.

Kilichotokea hapa ni kundi moja la hao lakini kila moja likifanya kazi kwa wakati wake na kundi jingine ni la wale waliodhani mambo yako safi lakini wakajikuta wakishtuliwa.

Katika hili, suala siyo Richmond na CCM ijiandae kwani baada ya suala la Richmond, yataibuka mambo mengi yatakayofanana na Richmond. Na kila moja litakuwa na mtikisiko wa aina yake. Kama tatizo lingekuwa Richmond, sasa tungekuwa tunaambiwa mmiliki wake na hata mmiliki wa Dowans tungekuwa tunamjua baada ya ripoti ya Kamati ya bunge.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi, siasa zake zimechafuka kweli kweli hali iliyolifanya bunge kuwa bunge la upinzani. Wapo wapinzani wa aina mbili; wale wa kawaida wa vyama, na wale wa ndani ya CCM ambao wanataka kujisafisha kwa wapiga kura wao.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwa sasa tutarajie wabunge hawa kujiandaa kukusanya heshima yao ya majimboni kwa kujionyesha uwezo wao wa kuichachafya serikali yao. Na haya yakitokea mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine wa serikali wataanza kufanya kazi zao kwa makini na kwa misingi ya sheria. Baadhi ya hizi sheria, ndiyo wabunge hawa wamekuwa wakizilalamikia kwamba zimepitwa na wakati. Kabla ya mapinduzi ya kikao cha bunge kilichopita, wabunge wangeweza kuivumilia serikali kama ingekunja sheria ili kuwezesha jambo fulani litekelezwe. Kwa sasa, itakuwa vigumu kwa sababu wabunge watakuwa macho kuangalia kitu chochote kinachokwenda kinyume na sheria. Watashambulia bila simile. Na hii itakuwa faraja kubwa kwa wabunge wa upinzani.

Kwa ujumla, bunge tangu lililopita hadi yajayo, ni mabunge ya upinzani. Wabunge wa CCM wanaona ufahari kujitambulisha na wabunge wa upinzani wakati katika kipindi kilichopita haikuwa hivyo. Wabunge wa CCM watataka kujionyesha kwamba wao ni wazalendo kwa kuwakumbatia na kuyakumbatia mawazo ya wapinzani. Ni kipindi cha neema kwa wapinzani iwapo watajipanga vizuri na wanaweza kuitumia kete hiyo katika majimbo.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema njia waliyoitafuta kwa muda wa miaka 16 sasa imewezeshwa na wana CCM wenyewe huku wapinzani wakichekelea.

Mwanasiasa mmoja wa upinzani, ametabiri kwamba katika hali kama hii, CCM haiwezi kutekeleza ahadi zake hata kwa asilimia 50 jambo litakalowafanya wapinzani kuibuka kidedea katika majimbo yao.

Kwa hali ilivyo sasa, wapinzani wachache waliomo bungeni, wamekwishajijengea mizizi kutokana na mambo yaliyopita. Hawana wasiwasi wa kupoteza majimbo yao.

Kwa upande wa CCM mambo ni tofauti kabisa. Hakuna nguvu ya pamoja tena kutokana na makundi yaliyomo. Wapo wachambuzi wa mambo wanaosema kwamba ushindi wa Kiteto unaonyesha njia nyeupe ya CCM kushinda katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, wachambuzi wengine wanasema Kiteto haiwezi kuwa kipimo kizuri kwa sababu ya mambo kadhaa. Kwanza nafasi hiyo ilikuwa ikijazwa ya mtu aliyefariki wa CCM. Hakuwapo ili kuhukumiwa na wananchi. Lakini ya pili, viongozi karibu wote walielekeza nguvu zao huko. Katika uchaguzi mkuu, kila mtu anakuwa katika jimbo lake akisulubiwa na wapiga kura wake.

Tatu kipindi cha miaka mitano kitakuwa kimepita, na ahadi za CCM ndiyo zitakuwa zikipimwa kama zimetekelezwa au la. Katika hali hiyo, wachambuzi wa mambo wanasema, CCM itakuwa na deni kwa wananchi ambalo itatakiwa kujibu.

Wachambuzi wa mambo wanasema uchaguzi mkuu ujao, utakuwa tofauti sana na uchaguzi wa miaka yote iliyopita kwa sababu ya watu kufunguka macho na uhuru wa watu kujieleza ambao umekuwa mpana katika kipindi cha awamu ya nne.

Hapo zamani, wachambuzi wanasema, wananchi walikuwa wakielezwa tu na wao kusikiliza, kupiga makofi au kuguna.

Lakini sasa, itakuwa ni zamu ya viongozi kueleza yale waliyoahidi na jinsi walivyoyatekeleza.

Hata hivyo, kiongozi mmoja wa upinzani, alipuuza mawazo kwamba upinzani nchini unaweza kuimarika kutokana na mgawanyiko ndani ya CCM.

"Kinachotokea ni kwamba CCM wanagombana wenyewe. Na ugomvi wao hautokani na tofauti ya ideology. Ni mambo yao tu ya mahusiano yao ndani ya chama. Ila kweli ninachokiona ni kwamba watapata taabu sana kutekeleza Ilani yao ya uchaguzi. Nakupa miaka mitatu, tuulizane,"alisema.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa Kiteto katika uchaguzi wa Jimbo hilo, alisema ni vigumu sana upinzani kufaidika na magomvi ya CCM kwa sababu vyama vya upinzani ni vichanga katika nyanja nyingi.

"Sioni ni kwa jinsi gani upinzani utakavyofanikiwa. Sioni fall out (anguko) ya CCM kwa sababu hawajatofautiana kiitikadi na kama wangetofautiana kiitikadi, basi ingekuwa rahisi kwao kudondoka na sisi kufaidi," alisema.

Akitolea mfano wa Kiteto, kiongozi huyo alisema CCM walishinda Kiteto kwa ubora wa mikakati na nguvu watu. "Sisi hatukuwa na human resources, hatukuwa na fedha wala mikakati. Tunafanya siasa katika old fashion (kizamani).

Kama tungeweza ku modernize opposition, tungeweza kufaidika na udhaifu huu wa CCM. Kwa kutumia uzoefu wao, CCM ikatumia kugawanyika kwa wana Kiteto kati ya wakulima na wafugaji na ikashinda,"alisema na kuongeza:

"Sisi tulijikita kwenye maeneo ya wakulima. CCM ikajikita katika maeneo ya wafugaji. Ikahakikisha kuwa iko na wafugaji. CCM ilikoshinda ilishinda kweli kweli. Kwa mfano kati Kata ya Ndedo CCM ilipata kura 992 na sisi tukapata kura 22. Kule Makami CCM walipata kura 940 na sisi tukapata 11.

Haya ni maeneo ya Wamasai hasa. Watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa zaidi ya asilimai 70. Kwa upande wetu, wapiga kura katika maeneo waliyotuunga mkono walikuwa wachache sana. Kwa mfano eneo moja, wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 11,000, waliojitokeza walikuwa 5,000. CHADEMA tukapata asilimia 56 tu. Kwenye wafugaji CCM iliwekeza na kushinda zaidi ya asilimia 80. Kwetu tulishinda lakini margin ndogo. CCM, ilijua waliojiandikisha. Sisi hatukujua," alisema na kuongeza kuwa heri ya vyama vya upinzani, ni kama makundi haya ya CCM yataamua kugawanyika na kuzaa chama kingine.

The only way ni sprit ya ccm kama matatizo ya sasa yatageuka kuwa ideological yawagawe katika makundi mawili. Au kungekuwa na high profile individual wakaingia kule.

Sentensi ya mwisho inanishawishi zaidi kuamini kwamba "mwandishi wetu" wa Rai si mtu mwandishi wa habari by profession bali mtoa mawazo ambaye jina limehifadhiwa na kuifanya makala hiyo kuwa leading story katika gazeti hilo.
 
Mlalahoi, hii habari (Makala) ya Rai ina maana kubwa sana kwa siasa za Tanzania na inajenga msingi wa kile ambacho kimekwisha kuzungumzwa humu JF na watu mbalimbali na Mwanakijiji aligusia alipozungumzia "Agenda 21". Kwa ujumla mambo ndio kwanza yanaanza na mtu mmoja nilimsikia akisema, "KUMEKUCHA" ama kweli kumekucha. Naamini ni lazima tuwe makini maana tunaweza kujikuta tunawekewa viongozi wale wale tunawatuhumu na SAFARI HII HAWATATUACHA WATATUMALIZA KWELI KWELI KABLA "HATUJAWALOWASSA".
 
Halisi,
Nikisoma katikati ya mistari naona RAI linajaribu kuwarudisha MAFISADI na WASAFI wa CCM kwenye mstari, kwa kisingizio cha ILANI ya Uchaguzi na ITIKADI ya CHAMA. RAI naona linajitahidi kuwataadharisha wana-CCM kuwa, kumsakama EL kwenye kadhia chafu ya UFISADI, kunaweza kupelekea kukigawanya CHAMA, hivyo lazima wabadilishe ajenda na mwelekeo kwenda kwenye utekelezaji wa ILANI kuwasahaulisha Watanzania machungu ya RICHMOND.
 
Back
Top Bottom