Ni uswahiba wa Manji uliomgharimu Prof. Kapuya uwaziri?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mmoja wa mawaziri wa muda mrefu hapa nchini Profesa Kapuya hayumo kwenye baraza la mawaziri na maswali ninayojiuliza ni uswahiba wake na Manji ndiyo umemgharimu..................Ni katika himaya ya Kapuya ambapo mwekezaji wa ndani Bw. Manji ameweza kufanya dili kubwa na NSSF na hivyo kujiongozea kipato chake kwenye mazingira tatanishi...................Je yawezekana hii ndiyo sababu JK na Pinda wake wakam'mwaga?

Au ni jinsi alivyoshughulikia migogoro ya wavuja jasho na kuacha taifa lina mpasuko mkubwa kati ya TUCTA na serikali ndivyo vimemponza mwanasiasa huyu mkongwe?

Lakini kule kwenye jimbo lake yamekuwepo malalamiko ya kuwajibu hovyo wapigakura kwa maswali mazito juu ya utendaji wa serikali na kauli zake za majibu ambazo hazikuwa zinalingana na umri wake au hata nyadhifa alizowahi kuzishika serikalini..........Je huenda nazo pia zimechangia au la.......................kama zipo sababu nyingine tuzichambue................
 
Manji ni swahiba wa Rais Kikwete na alimchangia pesa nyingi za kampeni ya Urais 2010 so Kapuya hana kosa hapo. Nachojua mie Kapuya na Kikwete walikuwa mabesti siku nyingi, labda kaamua kupumzika siasa ashuhulikie mgodi wake wa madini na bendi yake ya muziki.
 
he misled the fact to presda about Tucta against govt saga
 
Mnyamwezi huyo.

Waziri siku nyingi ila sijui kaisaidiaje Tabora.

Eti Waziri wa Kazi na wakati huo Wanyamwezi hatuna kazi.

Kijana wake ndiyo kwanza anarusha Risasi ovyo kama Rambo......

Vanyamwezi kazi kwelikweli...... :)



From = 3:00 >> .......... Politicians thank you father, For making them to be able
To lie with a straight face, While the nation cries.... They wanna thank you lord
 
Last edited by a moderator:
Manji ni swahiba wa Rais Kikwete na alimchangia pesa nyingi za kampeni ya Urais 2010 so Kapuya hana kosa hapo. Nachojua mie Kapuya na Kikwete walikuwa mabesti siku nyingi, labda kaamua kupumzika siasa ashuhulikie mgodi wake wa madini na bendi yake ya muziki.

He! Eti Kapuya ana bendi ya muziki wa dansi? Tafadhali naomba kujua jina la hiyo Bendi!
 
Back
Top Bottom