Ni ushauri gani umewahi kumpa mtu ukaleta matokeo ya faida au matatizo makubwa?

run CMD

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,798
3,109
Wakuu mambo vipi
Katika harakati za hapa na pale maisha unaweza kuchangia matokeo fulani kwa watu tunaoshirikiana nao.
Rafiki yangu mmoja aliniomba ushauri kuhusu kuoa (ingawa mwenyewe sijaoa ila nikatoa kama kocha hachezi ila ni mwalimu) nikampa ushauri huyo mwanamke yupo poa kabisa wewe komaa ila daah aliyokumbana nayo sasa baada ya kuoa nilijutia sana nabaki tu namuhurumia ...

karibuni wewe ulitoa ushauri gani ukaleta matokeo makubwa ambayo wewe hukutadhamia? Matokeo mazuri au mabaya!
 
Mambo Mazito sana Hasa nisiyo na ufahamu nayo,
Siombi wala kutoa ushauri.
 
Mimi ni bingwa wa kushauri watu hata yale siyawezi! Ila kuna wengi wananiamini sana huenda wamenufaika!
 
Sasa yaliyomkuta yapi hayo

Kwa nini usiweke wazi kwa faida ya wengi
 
Najuta kuwa sehemu ya watu tuliomshauri jiwe kuchukua form 2015
Kama ndiye ww, basi unastahili Award of the Century na tuzo maalum ya Udokta wa heshima katika fani ya unasihi. Ngoja nisevu jina lako, tutakuhitaji tena effectively 2025 ili tumrudishe Ikulu kwa awamu zingine nyingi tu ^ATAKE ASITAKE!^
 
😳 mtafute Nkamia atakusaidia sio mimi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom