Ni usemi upi umekugusa?? Na kwanini??

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
NI USEMI UPI UMEKUKAMATA?:

1. "Kuzaliwa masikini siyo kosa lako,ila kufa masikini ni ujinga wako." ~ Bill Gate

2. "Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa." ~ Felix Bundala

3. "Heri kufa na mawazo yanayoishi, kuliko kuishi na Mawazo yaliyokufa." ~ Che Guevara

4. "Vita inamalizwa kwa vita na ili tuachane na matumizi ya bunduki inabidi itumike bunduki." ~ Mao ze Dong

5. "Sitamani kumjua babu yangu alikuwa nani, ninachotaka kumfahamu mjukuu wake atakuwa na tabia gani." ~ Martin Luther King

6. "Usimuulize mtu yoyote anayenijua mimi maana utamjua yeye kupitia mimi." Joe Lescot

7. "Muonekano siku zote hutengeneza uwezekano." ~ Lucky Crackent

8. "Hatuwapendi wanawake kwa sababu ni wazuri, ila tunawaona wazuri kwa sababu tunawapenda." ~ Luck Crackent

9. "Watu ni wengi ila binadamu ni wachache." ~ Fidel Castro

10. "Usiishi kwa sababu unaishi, tafuta sababu ya wewe kuishi." ~ Jay Ozil Cazorla Wilshere

11. "Hakuna mkate mgumu mbele ya chai." ~ Bob Sydou

12. "Kichwa kikubwa bila Akili ni Adhabu kwa miguu." ~ Thabiti Kube..
 
Kabla ya kuangalia mafanikio yako fikiria kwanza thamani yako.

Maisha siyo mashindano ya mbio bali ni safari, hivyo kufika kabla ya Mwenzio ina maana ndogo katika maisha.
 
Msemo naoukubali ni huu tu "Mipango bila pesa ni kelele"
 
Back
Top Bottom