mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,843
- 3,128
Nimekua nikifuatilia threads na comments mbalimbali za wadau,hasa wale mahasimu wa Rais Magufuli.
Sipendi kutumia neno beberu,ila acha nilitumie kwa leo.
Baadhi ya watanzania wakisikia matamko ya mabeberu hasa yale negative kuhusu utawala wa nchi ,hukenua meno na kushangilia kwa nguvu zote,wakiombea majanga yatokee.
Nchi ikikwama tumekwama wananchi,sio Magufuli,nchi ikikosa misaada wanaoathirika ni raia wa chini kimaisha.
Mnaoshangilia na kuombea nchi itengwe mlikwisha jiandaa?.,ndio maana mnavuruga kila uchao?
Nasikia wengine mmeandaliwa katika huu mkutano wa sadc muinue mabango yenu ili yamulikwe na wafadhili wa huu mchezo wenu ,kama ni kweli nyie ni wakuogopwa kama ukoma.
Tanzania ndio nchi yetu,hakuna pa kukimbilia mambo yakiharibika ,jifunzeni kwa baadhi ya nchi,waliharibu nchi zao kwa mikono yao na leo wanajuta,neno ningelijua huja baadae.