Ni Upuuzi Polisi na Mgambo kuwasumbua vijana mtaani eti kisa kitambulisho cha Machinga

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Nimenyamaza sana ila naomba niongee ili swala la vitambulisho haiwezekani kila mtu akawa na kitambulisho mi nakataa

Polisi kwa kushirikiana na mgambo wanakamata vijana mtaani eti kisa vitambulisho vya elfu 20...

Mmeshindwa kutoa ajira kwa vijana sasa mnalazimisha kila mtu awe machinga ...

Vijana wamejaa mtaani kazi hakuna makampuni hayatoi kazi kwa sababu ya sera mbovu za utawala wa kidicteta na ubabe...

Vile viwanda viko wapi muwakamate vijana kuwapeleka kufanya kazi uko?

Ile milioni 50 kila kijiji iko wapi wapewe vijana ndio wawe machinga ..

Mtu hana hata mtaji yaani day waka kwa siku anatafuta buku 2 apate msosi kwa mama ntilie wewe unamkamata unamsumbua unamuweka ndani kwa sababu hana kitambulisho..

Mtu hana pesa ya kula ya kitambulisho anapata wapi ..

Magufuli acha kuonea vijana nakusema wewe kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya wanatekeleza matamshi yako ..

wanatesa vijana mtaani mimi nasema tupo kwenye nchi huru kila mtu awe na uhuru wake wa kufanya chochote bila kuingiliwa sio unamkuta kijana kakaa unampeleka police eti hana kitambulisho?..

Tunataka kutengeneza taifa la machinga upuuzi mtupu ninaposema hivi kuna vijana nimetoka leo kuwatoa ndani walikamatwa jana kisa hawana vitambulisho vya machinga ..

Huu ni upuuzi na ni hatari kwa usalama wa taifa acheni Longolongo wapeni vijana kazi, fungueni hivyo viwanda tuvione , toeni milion 50 kila kijiji ...

Huu utoto na laana ya kuwakamata wamama hadi wauza kalanga itawagarimu sana

Serikali hii inaonekana imelaniwa vilivyo.
 
Ukitaka kucheka sasa fuatilia hiyo pesa ujue inaingia mfuko gani hapo ndio utafurahi. Hakuna receipt ya EFD wala nini. Nani anakagua matumizi ya hiyo hela hafahamiki. Wabunge wako kimya huku watu wakilipishwa hela kwa nguvu bila ridhaa yao.
Magufuli kwa kweli anaonea vijana duh .

Sasa hvi imekuwa kuishi kwa hofu mtaani..

Halafu jamaa linakwambia serikali ya wanyonge
 
Kwanza inatakiwa wakuambie kwa Sheria ipi unaniuzia karatasi ya sh 2000 kwa elf 20,pia wanayo risiti tumeambiwa tudai risiti,Tatu wanipe akaunti nikalipie bank,NNE wanipeleke mahakamani ndo ikaamue kama ni kosa kutokuwa nacho.From Milioni 50 kila kijiji to elf20 kila mwanakijiji, tunaelekea vizuri kwa kweli. Ukisomesha watu no ni lzm nawe uisome ni kanuni. Zaidi ni janjajanja ya wachache kutumia fursa maana kuingia polisi ni bure kutoka lzm ulipie kukamatwa kwako.
 
Vijana fanyeni kazi acheni kupenda bata, uvivu usanii ubishoo udalali na kulia lia, kama huna buku 20 na hutaki usumbufu na ni jobless asa unafanya nini mjini? Si uende bush kulima hata kwa meno kama jembe huna? Hakuna nchi duniani yenye maendeleo bila kukamua wananchi wake kodi!!! Kaisake mtandaoni ukiipata nakulipia hiyo buku ishirini na wenzako wote mdamkie kwangu, first come first served!!!!, machinga ni kazi nzuri unajiajiri unajilipa mshahara unaamka na kulala unavyotaka ukiamua kuchill no stress, ukikaa home wiki nzima na bata zako no warning letter! Mimi ni Machinga na maisha mbona fresh tu mi siendekezi maisha feki ya instagram, sihitaji kiki wala ubishoo nakula kwa jasho nawewe na vijana wako uliowatoa lupango mkiamua mnaweza!!! Nasema hili lifuatalo kwa Dhati ya moyo wangu , what you guys need is a “twist of your minds””
Hivi Bush ndio wanaishi wasio na kazi ni kijiji gani icho na kiko wapi?.
 
Wameshakuona, ukuu wa wilaya uko mbioni.
Vijana fanyeni kazi acheni kupenda bata, uvivu usanii ubishoo udalali na kulia lia, kama huna buku 20 na hutaki usumbufu na ni jobless asa unafanya nini mjini? Si uende bush kulima hata kwa meno kama jembe huna? Hakuna nchi duniani yenye maendeleo bila kukamua wananchi wake kodi!!! Kaisake mtandaoni ukiipata nakulipia hiyo buku ishirini na wenzako wote mdamkie kwangu, first come first served!!!!, machinga ni kazi nzuri unajiajiri unajilipa mshahara unaamka na kulala unavyotaka ukiamua kuchill no stress, ukikaa home wiki nzima na bata zako no warning letter! Mimi ni Machinga na maisha mbona fresh tu mi siendekezi maisha feki ya instagram, sihitaji kiki wala ubishoo nakula kwa jasho nawewe na vijana wako uliowatoa lupango mkiamua mnaweza!!! Nasema hili lifuatalo kwa Dhati ya moyo wangu , what you guys need is a “twist of your minds””, haki ya Mungu nakupa ushuhuda mimi kila nikibanwa na maisha natwist mind napiga kazi yoyote mbele yangu siangalii elimu yangu sijali wajinga wanaonicheka ila wanangu wanakula!!! And that makes me very happy indeed!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bush ni kule walikotoka wazee wa kila kijana ambako kuna mashamba yanajaa Nyasi tu kwa maana vijana wako mjini bize na kupost Mapicha ya ovyo Instagram kuimba bongofleva , udalali kupiga mizinga na kuekti muvi na Komedi bila kusahau mikeka ya kubeti! Bado kidogo tu Mzee atafanikiwa kuondoa kizazi cha watu wavivu, mwakani iwe buku 50 ili tukimbilie majembe!!!
Kwahiyo solution ni kuwa na kitambulisho cha elf 20?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimenyamaza sana ila naomba niongee ili swala la vitambulisho haiwezekani kila mtu akawa na kitambulisho mi nakataa

Polisi kwa kushirikiana na mgambo wanakamata vijana mtaani eti kisa vitambulisho vya elfu 20...

Mmeshindwa kutoa ajira kwa vijana sasa mnalazimisha kila mtu awe machinga ...

Vijana wamejaa mtaani kazi hakuna makampuni hayatoi kazi kwa sababu ya sera mbovu za utawala wa kidicteta na ubabe...

Vile viwanda viko wapi muwakamate vijana kuwapeleka kufanya kazi uko?

Ile milioni 50 kila kijiji iko wapi wapewe vijana ndio wawe machinga ..

Mtu hana hata mtaji yaani day waka kwa siku anatafuta buku 2 apate msosi kwa mama ntilie wewe unamkamata unamsumbua unamuweka ndani kwa sababu hana kitambulisho..

Mtu hana pesa ya kula ya kitambulisho anapata wapi ..

Magufuli acha kuonea vijana nakusema wewe kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya wanatekeleza matamshi yako ..

wanatesa vijana mtaani mimi nasema tupo kwenye nchi huru kila mtu awe na uhuru wake wa kufanya chochote bila kuingiliwa sio unamkuta kijana kakaa unampeleka police eti hana kitambulisho?..

Tunataka kutengeneza taifa la machinga upuuzi mtupu ninaposema hivi kuna vijana nimetoka leo kuwatoa ndani walikamatwa jana kisa hawana vitambulisho vya machinga ..

Huu ni upuuzi na ni hatari kwa usalama wa taifa acheni Longolongo wapeni vijana kazi, fungueni hivyo viwanda tuvione , toeni milion 50 kila kijiji ...

Huu utoto na laana ya kuwakamata wamama hadi wauza kalanga itawagarimu sana

Serikali hii inaonekana imelaniwa vilivyo.
Uko sahihi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko us afu watuponda na hujui tunavyoishi huku...ulichonishangaza ni kua hujui kama hakuna nchi ambayo haina vijana wasio fanya kazi (unemployment) na c kwa hiari yao bali wanakosa wanachotaka
Niko US mzee sihitaji madafu nakuapia haki ya Mungu nimesahau kushika madafu, i just believe in new regime! Inanyoosha kwelikweli wavivu na Wezi wote!! Na ni wakati huu tu nchi itapiga hatua believe me or not! Namuomba Mzee akaze zaidi Mungu yu pamoja nae we hata hujashangaa miaka 39 tulishindwa Afcon na sasa kaingia tu “SASA NI ZAMU YETU AFCON”? Hujiulizi kwa nini ni leo sio jana na juzi? Unataka malaika wakushukie wakwambie ulipe kodi zijenge SGR?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kucheka sasa fuatilia hiyo pesa ujue inaingia mfuko gani hapo ndio utafurahi. Hakuna receipt ya EFD wala nini. Nani anakagua matumizi ya hiyo hela hafahamiki. Wabunge wako kimya huku watu wakilipishwa hela kwa nguvu bila ridhaa yao.
Aiseee !!!
 
Vijana fanyeni kazi acheni kupenda bata, uvivu usanii ubishoo udalali na kulia lia, kama huna buku 20 na hutaki usumbufu na ni jobless asa unafanya nini mjini? Si uende bush kusaidiana kulima na wazee hata kwa meno ikibidi kama majembe hakuna? Hakuna nchi duniani yenye maendeleo bila kukamua wananchi wake kodi!!! Kaisake mtandaoni ukiipata nakulipia hiyo buku ishirini na wenzako wote mdamkie kwangu, first come first served!!!!, machinga mbona ni kazi nzuri tu unajiajiri unajilipa mshahara unaamka na kulala unavyotaka ukiamua kuchill no stress, ukikaa home wiki nzima na bata zako no warning letter! Mimi ni Machinga na maisha mbona fresh tu mi siendekezi maisha feki ya instagram, sihitaji kiki wala ubishoo nakula kwa jasho nawewe na vijana wako uliowatoa lupango mkiamua mnaweza!!! Nasema hili lifuatalo kwa Dhati ya moyo wangu , what you guys need is a “twist of your minds””, haki ya Mungu nakupa ushuhuda mimi kila nikibanwa na maisha natwist mind napiga kazi yoyote mbele yangu siangalii elimu yangu sijali wajinga wanaonicheka ila wanangu wanavaa wanakula!!! And that makes me very happy indeed!!!
YOU ARE A FOOL.
 
Niko US mzee sihitaji madafu nakuapia haki ya Mungu nimesahau kushika madafu, i just believe in new regime! Inanyoosha kwelikweli wavivu na Wezi wote!! Na ni wakati huu tu nchi itapiga hatua believe me or not! Namuomba Mzee akaze zaidi Mungu yu pamoja nae we hata hujashangaa miaka 39 tulishindwa Afcon na sasa kaingia tu “SASA NI ZAMU YETU AFCON”? Hujiulizi kwa nini ni leo sio jana na juzi? Unataka malaika wakushukie wakwambie ulipe kodi zijenge SGR?
Mara wewe ni machinga, mara uko US!! Au unadanga?
 
Viazi viko aina nyingi mbatata viazi mviringo vyeupe viazi mviringo vyekundu viazi vitamu vyeupe viazi vitamu vyekundu viazi vikuu, viazi ulaya . Sasa sijui ulimaanisha mi ni kiazi gani japo napenda niwe kiazi kikuu au vipi? Gharama ya kulima ni jembe na msuli wako tu!! Naona umeshindwa hoja umeanza kashfa!!! Nadhani nimekuzidi IQ bila shaka umeshagundua inside your head!! Ha haha!!!
Huo msuli unalima heka ngapi?
 
Back
Top Bottom