Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, May 2, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pale Lumumba kulikuwa na kitengo cha propaganda, kwa watanzania wengi propaganda ni uongo. Moja ya kazi ya kitengo kile ilikuwa kuwaeleza watanzania uongo dhidi ya vyama vya upinzani kuhusu ukabila, udini na ukanda ambao kwa kipindi hicho uliwaingia barabara na ndio matokeo ya CUF chama cha waislamu na CDM cha wakristo.

  Katika pitapita yangu kwenye thread moja hapa ndani ya JF niwekutana na majina ya watu ambao wanataka kurudisha CDM kwenye uongo ule ule bila wao kujitambua. Ni upuuzi mkubwa kugawa nchi kikanda, kidini na kikabila hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania tunashauku kubwa ya mabadiliko. Taifa hili halikupigania uhuru kwa kuwabagua watu wa kusini, kanda ya kati au pwani eti kwa sababu wapo wachache na waislamu. Kumbuka katika uchaguzi hatutazami tu idadi ya watu katika maeneo husika ila tunatazama idadi ya watu walijiandikisha kupiga kura na ushiriki wao kwenye kupiga kura.

  Kuwa na mtazamo kwamba kanda ya ziwa na kaskazini pekee ndiyo wanaoweza kuiangusha CCM ni upuuzi. Tunachopaswa kutambua ni kwamba lazima uamsho huu ufanywe kwa Watanzania wote bila kujali dini,ukanda na ukabila. Nguvu ya umma (without discrimination za ukanda,udini na ukabila) ndio itakayotupa uhuru ya pili wa taifa letu (i.e. uhuru wa kifikra kuondokana na ukoloni mweusi ndani ya Taifa letu)

  Mabadiliko hayawezi kuwa na tija kwa mantiki ya kugawanya nchi yetu ya Tanzania katika makundi.Tunajenga mitazamo ileile ambayo CDM wanaikimbia kutokana na propaganda za kipindi cha miaka ya nyuma. CDM hakijadominate kanda ya pwani si kwa sababu ya waislamu wengi bali nia kwa sababu hakijawekeza nguvu ya kutosha kutoa elimu ya uraia.Suala la msingi hapa ni kwa jinsi gani CDM wanatakiwa kujipanga.Kwa mitazamo ya kibaguzi tutajenga imani kwamba maeneo ambayo CHADEMA inaungwa mkono ni maeneo yenye wakristo wengi na hivyo kuwatenga waislamu, na hii ni hatari,lazima tuwekeze kwenye fikra tulivu kutatua changamoto katika maeneo ambayo bado siasa ya CDM haijakubalika na majority.


  Lakini villevile tutambue kwamba hatuwezi kuwa na raisi toka CDM na kufanya kazi kwa ufanisi bila kuwa na wabunge wa kutosha hivyo kuna majukumu makuu mawili: Kuhakikisha hatupotezi wabunge tulio nao sasa na kuongeza idadi ya wabunge.


  Nawakilisha
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Umenena vyema ccm wanajaribu kutumia propaganda ya udini kuibomoa CDM lakini ukweli ni kwamba CDM wanapaswa kuwekeza nguvu zaidi kanda za mashariki, kati, kusini na hata magharibi bila kusahau Zanzibar. Hakuna ubishi kwamba propaganda za udini za ccm zimefeli na hili lilithibitika katika uchaguzi wa igunga ambapo dhana ya udini ilitawala lakini wana igunga walionesha kwamba hawatishwi na propaganda hizo japokuwa CDM hawakushinda lakini bado maergin ilikuwa ndogo sana tofauti na ilivyofikiliwa awali hasa ukizingatia tabora ilikuwa ngome ya CCM na CUF. Nina hakika bila shaka kama CDM watawekeza nguvu zaidi igunga na kuweka mgombea ambaye ana sura ya ki- chadema kwa maana mwenye uwezo wa kujenga hoja na kulitawala jukwaa kama walivyo wabunge wengi wa CDM basi igunga na majimbo mengine mengi tu yataangukia mikononi mwa CDM mwaka 2015.
   
 3. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna chama cha waislamu wala cha wakristu.
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii thread ni kwa ajili ya Wana-Chadema tu au hata tusio na vyama twaweza kuchangia?
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Udini ni hoja muflisi kabisa. JK na CCM yake ndio wanaipandikiza
   
 6. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  KUDOS mkuu, umeongea point za msingi sana...naamini sana katika umoja na mshikamano ndani ya jamii katika misingi ya UTAIFA na sio ethnicity so umenikuna sana uliposema "Nguvu ya umma (without discrimination za ukanda,udini na ukabila) ndio itakayotupa uhuru ya pili wa taifa letu (i.e. uhuru wa kifikra kuondokana na ukoloni mweusi ndani ya Taifa letu"
   
 7. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakika uko sahihi Mkuu....jukumu kubwa ni kuondoa mentality hizi kwa baadhi ya maeneo ya Tafa letu kwa misingi ya fikra tulivu.
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Nchi hii ipo kikanda na itaendelea kuwa kikanda. Chadema ni chama cha kanda ya kaskazini. Hebu angalia mfano huu, kanda ya ziwa hakuna hata chuo kikuu cha serikali hata kimoja, unadhani nini hapo kama sio ukanda? angalia hii pia, kwa nini viongozi wakuu wa chadema i.e mwenyekiti na katibu, wote ni wa kanda ya kaskazini?.
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi hoja ya mwenyekiti mbowe ya kugawa nchi kwa ukanda siungi mkono.
   
 10. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuwa na IMANI maana yake sio kuwa Mkristo au Muislamu...hata Wapagani wana-IMANI, there is no way 100% unaweza kukwepa siasa. Ni watanzania wachache sana waliokuwa wanajua definition nzuri ya siasa, wengi wao walijua kwamba siasa ni uzushi, utapeli, mchezo mchafu n.k. Lakini unapoongelea siasa kwa Mmarekani lazima ujikite kwenye uchumi na teknolojia...kwa mtanzania ni majungu, matusi, n.k. na chimbuko la mentality hizi ni kitengo cha propaganda kilichokwepo pale Lumumba. Hivyo lazima tutambue kwamba siasa ni ujuzi na maarifa ambayo huweka misingi imara ya mafanikio katika jamii, hivyo wewe ni sehemu ya siasa na unaruhusiwa kuchangia.
   
 11. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mantiki hii, kwasababu Raisi,Makamu wa Raisi, Raisi wa Zanzibar, Raisi wa kwanza na wa pili wa Zanzibar ni waislamu. Je nchi ya Tanzania ni ya ki-islamu. Fikra tulivu ndio njia ya maamuzi sahihi.TAFAKARI!
   
 12. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Suala la ukanda lipo leo vurugu ilitokea tandahimba Cdm haijalaan hata kidogo lakin kavurugu kidogo katokee arusha mtawasikia nchi haitatawarika
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hivi mwaka 2015 cdm wakishinda bara ccm ikashinda zanzibar itakuaje?? au cdm wapate bara cuf wachukue zenji...serikali mbili zenye vyama tofauti sera tofauti zitawezaje kufanya kazi pamoja?? au ndo muungano utakua ni bye bye hapo
   
 14. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Kwani chadema wakichukua nchi wasivoipenda zenji watavunja muungano maramoja,
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Acha ndoto muungano uvunjike mara ngapi?
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  sasa kama umeshavunjika kwanini unachangia humu jamvini wakati kwenu ni zenji?
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Facts are sturbon things na huu ni ukweli mchungu ambao Watanzania lazima tuukubali, tuumeze ndipo tusonge mbele!.

  Unamaanisha Chadema wakijipanga watazoa kura Pemba?. Jee unazijua sababu zinazopelekea CCM kushindwa kupata hata kiti kimoja Pemba?. Kwa hiyo Chadema wakijipanga watavuna majimbo Pemba!.

  Hivi unayo taarifaa kama sio Nyerere kufuta mitihani ya Cambridge kwa pass mark moja nchi nzima, shule zote za sekondari na vyuo vyote vingejaa watu wa makabila fulani fulani tuu?!. Na kuna makabila fulani fulani wangeishia shule za msingi tuu! Utake usitake sababu zipo na ni facts!. You can't deny facts!. Jee hizo sababu ni za kipuuzi?.

  Sisi sote ni Watanzania na nchi yetu ni moja, jee unajua kuna watu wa dini fulani fulani wamepata fursa za kujiendeleza kielimu kuliko dini fulani fulani?. Unazijua sababu?. Sababu hizo ni facts!. Jee nazo ni upuuzi?.

  Unajua moto nyikani huanza vipi?. Siku zote moto wa nyika huanzishwa na cheche moja tuu na kuenezwa na upepo. Unajua cheche ikianzia upande tofouti na upepo unavyovuma moto huo huzimika papo hapo!.

  Kwenye siasa kuna kitu kinaitwa ngome. Ngome ndipo pale ambapo umeota mizizi na unapoanzishia cheche ya moto wa nyika yako ambapo utasambaa!.

  CUF wana ngome yao na mtaji wao waliowekeza na ndio maana wanavuna walichopanda!. CDM nao wana ngome yao na mtaji wao ni watu. CCM kwa vile kilikuwa chama tawala chenyewe kote ni ngome zake na mtaji wake ni mtandao wake ulioenea hadi vijijini. Ili kuleta mageuzi ya kweli ni lazima waokombe huo mtaji wa CCM na ili kuukomba lazima moto wako ukauanzishie kwenye ngome yako ndipo usambae kote!.

  Kubali kataa siasa za ukabila zipo ndio maana kuna makabila fulani hawawezi kuukwa urais wa nchi hii no matter how good they are!.

  Huu sio uongo ni bitter truth ambazo lazima tukabiliane nazo kwa kuzi face na sio ni deny kwa kukanusha as if they don't exist!.

  Lets face the bitter truth kwa kumeza the bitter pill ili kuutibu huu ugonjwa wa ukanda, udini na ukabila!.

  Mimi binafsi ni muumini wa ukweli na hivyo naamini ukanda, ukabila na udini, upo kwenye siasa za Tanzania na dawa yake ni to set a thief to catch a thief, tuutumie ukabila huo huo, udini huo huo na ukanda huo huo kuutibu ugonjwa huo huo!.

  Pasco!.
   
 18. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Pasco naona umekuwa mkaali unamtishia mtoa mada!

  Kuanzisha chama sehemu fulani hakufanyi chama kiwe cha kikanda au kabila la sehemu husika!

  Kuwa na base sehemu fulani haina maana kule kwenye base utumie dini au kabila la eneo hilo kusimika mizizi yako!

  Kuna mambo umechanganya mkuu wangu labda kwa kuwa una hasira na neno "UPUUZI" lililotumiwa na muwanzisha mada.

  Kuleta case ya pemba-CUF kama model ni udhaifu mkubwa uliouonyesha kwa kuwa pemba-cuf vs unguja-CCM kuna

  historia yake, tumia akili sio jazba, hiyo case haifanani kabisa na CDM-Kaskazini.
   
 19. f

  fat faza Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo umenena mkuu... kama huna uwezo usitafute sababu ya kuficha udhaifu wako
   
 20. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Pasco, unatakiwa kutumia fikra tulivu kujibu umantiki wa hoja, wewe unachojaribu ni kuzidi kujenga mentality za kidini na kikabila bila kujua mwathirika namba moja ni wewe, siasa huenda sambamba na nyakati, umesema "Ili kuleta mageuzi ya kweli ni lazima waokombe huo mtaji wa CCM na ili kuukomba lazima moto wako ukauanzishie kwenye ngome yako ndipo usambae kote!" Kwa maneno haya ni lazima CDM wapeleke uamsho nchi nzima kuepusha fikra za kibaguzi kama za kwako.
   
Loading...