Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kumekuwa na upotoshwaji mkubwa kutoka kwa wale wanazoziendesha nchi zao kiimla na kujitetea kuwa demokrasia siyo sawa sawa na kinywaji cha coca-cola ambapo radha yake itakuwa moja Dunia nzima.
Tafsiri sahihi ni kuwa demokrasia ni moja Dunia nzima na ni serikali ya wananchi, iliyochaguliwa na wananchi hao Katika uchaguzi uliokuwa huru na wa Haki, ambapo viongozi waliochaguliwa wanabeba dhamana kuwatumikia wananchi hao kwa usawa.
Hii kauli ya kujitetea kuwa demokrassia siyo sawaswa na coca-cola, inatolewa na viongozi wa kiimla, ambapo ilianza kutolewa na Mwendazake na sasa inaendelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Hivi wewe uliwahi kuona wapi, nchi inayoongozwa kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi, chama tawala ndiyo pekee kiwe na uhuru wa kufanya vikao vyake itakavyo na vyama vingine vya upinzani, vizuiliwe na Jeshi la Polisi kwa kutolewa sababu ambazo hazina ukweli wowote??
Dawa ni moja tu kwa nchi yetu, kupata Katiba mpya ya nchi, ambayo italeta usawa wa namna ya kuendesha shughuli za kisiasa nchini. Full Stop,