Ni upi muda unaotakiwa kuoa tena ikiwa utafiwa na mke

mkuu pole sana...........wala usijali hao watoto watakuwa we walee kwanza wakue na wapate ufahamu mzuri........

NB: sikiliza moyo wako unasema
 
Tulia kwanza ipite hata miaka mitatu ;Ishu mke na ishu ya ulezi ni vitu viwili tofauti;Wewe unadhani ukioa ndiyo watoto wako watalelewa vizuri lakini mkuu inawezekana mambo yakawa kinyume na unavyofikiri,huyo mke anaweza kukusambaratisha wewe na watoto wako.Nakushauri ulee watoto wako Mungu atakupa maarifa na uwezo wa kuwalea ,Pia waweza kumpata hata ndugu mwanamke mtu mzima watoto wakishakuwa ndio utafute mke.
 
Dah, pole mkuu, najua inaumiza kwa namna ambayo haielezeki. Cha muhimu tulia jipe mda hadi pale utakapoona umetulia. Upatapo tatizo usipende kuwaza au kusema 'mke wangu angekuwepo, ....', itakuumiza sana.
Kwa kuwa watoto ni wakubwa, miaka kumi na mwingine sita, hao kwa sasa sidhani kama ni shida sana.
Kwa mara nyingine pole mkuu.
 
Back
Top Bottom