Ni upi msimamo wa Serikali yetu kuhusu mustakabali wa mazingira ya nchi?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,514
2,000
Naomba anayeujua msimamo wa Serikali yetu kuhusu mustakabali wa mazingira ya Tanzania atusaidie tafadhali?

Rais ameshasema asingependa kuona mtu aliyelima ndani ya eneo la mto (linanolozuiwa kisheria za Tanzania na kimataifa) ang’olewe mazao yake. Hapana shaka, wananchi zaidi watavamia vyanzo vya maji na kwa kuwa agizo ni la Rais, hakuna atakayethubutu kuwazuia.


Ameagiza wananchi waliovamia na kuanzisha makazi katika mapori ya hifadhi wasiondoshwe. Nimemsikia akiagiza hata mbuga za wanyama ambazo wanyama hawatembelei sana zigawiwe kwa watu! (Kama nilimsikia vibaya naomba nisahihishwe). Kasi ya Serikali ya kupanga na kupima viwanja imepitwa mbali sana na kasi ya wananchi wanaojijengea kiholela. Imefika mahali, Serikali imenyoosha mikono na kusema kuwa haitambomolea mtu isipokuwa itatoa hati tu ili ikusanye kodi.

Wakati huohuo, Dar es Salaam inunuka! Pamoja mandhari inayolipa nafasi ya kuwa moja kati ya majiji ya kuvutia kabisa duniani, Dar imeorodheshwa kama jiji la 14 uchafu kabisa duniani! Halmashauri zake zinalemewa na mzigo wa taka zikiwa na uwezo wa kukusanya asilimia 40 tu ya taka zote zinazozalishwa. Hakuna mpango, elimu wala seria zinazowataka wazalishaji wa taka kuchambua aina za taka kabla hazijazolewa kama wananchi wa nchi zingine wafanyavyo.

Baada ya kutathmini madhara yake, nchi nyingi zimeanza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Tanzania matumizi ya mifuko ndo kwanza yanaongezeka: Tanzania mfuko wa plastiki ni mfuo kweli lakini pia, ni mafuta ya kuwashia jiko, ni sahani ya chakula kwa mama ntilie, ni “Mobile tolet”…matokeo yake, bahari na fukwe zetu zimegeuka dampo kubwa la taka za plastiki.

Niwaulize sasa, baadhi ya wachangiaji humu mitandaoni ambao wameonyesha matumaini na uelewa mkubwa kuhusu utendaji wa Serikali yetu; Nini hatma ya mazingira ya Tanzania?
By, James Gayo -Cartoonist.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom