Ni upande upi unahusika na uandaaji mikataba kati ya serikali na mwekezaji?

Alhandro

Member
Jun 2, 2011
94
18
Wanajukwaa kheri?

Naomba nianze moja kwa moja kwa kujikita katika suala hili la uandaaji mikataba baina ya serikali na mwekezaji. Hii inatokana na haya yanayo jili kila uchao na uchwao inapokuja issue ya upande mmoja wapo kutoafikiana na kitendekacho kuhusiana na shughuli kazi uliyo tiliwa mkataba.

Hivi unapo kuwa ukimtafuta mwekezaji mwekezaji akitafuta mahala pa kuwekeza ni wewe mwenye kazi unatakiwa kuandaa mkataba wa kazi husika iwapo utaridhika na vigezo vya utendaji kazi wake ama ni yeye wakati anatafuta kazi anakuja na mkataba wake ambao unapaswa kuufuata iwapo utaafikiana na ufanisi wa kazi yake?

Kama ni wewe mwenye tender ndiyo mhusika mkuu wa uandaaji huo,inakuwaje unaandaa mkataba ambao kesho na kesho kutwa usipo ridhika na ufanisi wake kila ukijaribu kujinasua nao wewe ndiyo unakuwa mhanga?

Ina maana umeandaa mkataba ambao hata wewe mwenyewe unashindwa kujinasua kila uonapo mambo hayajaenda sawa!? Au tuseme umeandaa mkataba ambao hata wewe huujui madhara yake na faida zake?

Sipendi kuamini kwamba ni kweli unaweza ukaandaa mkataba mpaka kuuwasisilisha kwa mwekezaji na mkasainiana ilhali hata wewe mwenyewe huujui kiundani. Ama tuseme waandaaji hawa wa mkataba wanastahili kutiliwa shaka juu yake kwani waweza kuwa wanufaika wayo pia?

Na siwezi amini kama kweli mwekezaji ndiye anatembea na makaraburasha ya kutafuta tenda pamoja mkataba kabisa ambapo sisi kazi yetu tukisha afiki kumpa tenda basi ni kusaini tu kazi inaendelea. Hata kama ndivyo, ina maana hata hatujihangaishi kuipitia kuona sehemu zinazo toa nafuu kwetu wenye mali hata ikionekana mwekezaji katenda kinyume chake?

Kama waandaaji munayafanya haya kwa ustadi,iweje kila mikataba inayo onekana kazi zake kwenda visivyo ikivunjwa tu na wahusika kwenda mahakamni basi tuna asilimia kubwa ya kushindwa?

Naombeni msaada kuhusu hili jamani maana limekuwa likinitesa kila nifikiriapo pindi niwazapo juu ya hukumu zitolewazo juu yetu. Unaweza mlaumu mwanasheria aliye simamia shitaka kumbe msingi wa shitaka husika ndiyo umesha imaliza kesi yenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom