Ni unafiki au kutojikubali

ISSA SHARAFI

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
407
75
Habari za saa hizi wanajamvi
Iko hv ktk hali ya kushangaza kwa watanzania ni pale mtu anapoongea lugha ya kiingereza anajihisi kma shujaa aliyemwondoa Gaddaf madarakan kuliko pale anapotumia lugha ya kiswahili.
Inaonekana wazi kwamba kiswahili sasa kmekua ni lugha ya watu wasienda shule. Kwann tumepoteza uzalendo wa kuthamini lugha yetu.
Tuangalie watu kma wachina ambao kwa asilimia kubwa hutumia lugha yao ktk mambo yao yote pia kuna nchi kma Hispania, Brazil ambako watu wake wengi hawajui kiingereza, lkn imekuwa tofauti kwa hapa nyumbani yaani mtu akiongea kiswahili:eek: bila kuweka neno la kizungu bac anajioona kma kakosea na kudharaulika.
Kiukweli tumejisahau juu uthamini wa lugha yetu ya kiswahili kwn ni kitu kmojawapo ambacho kinaweza kuleta maendeleo ya taifa ktk suala zima la mawasiliano.
Watanzania tuikubali lugha yetu ya kiswahili na tujikubali wenyewe kukuza na kuindeleza lugha hii.

KISWAHILI NI LUGHA YETU NA TANZANIA NCHI YETU.
 
Umesema vyema mkuu. Hata mimi huwa nakerwa sana na tabia ya kuchanganya lugha mbili kwa maramoja,hasa kwenye kuongea. Sijui tunaelekea wapi na kiswahili chetu.
 
Back
Top Bottom