Ni umri gani hutakiwi kuvuka kabla ya kupata mtoto wa kwanza?

Mkuu lakini 40 years kwa jamii zetu za kiafrika huoni kama utakuwa umechelewa mathalani unastaafu una miaka 60 mtoto bado ana miaka 20 huoni kama pension yako itatumika kumsomesha mtoto na kutunza familia badala ya kuifaidi uzeeni kwako
Tusikariri muajiriwa tujifunze kujiajiri kama watu wa Asia
 
Wewe unajidanganya... sababu zinazolazimisha umri ufikiriwe ni uwezo wa kumtunza huku bado una nguvu za kufanya hivyo.. Ishu siyo kuzaa tu... UNLESS UWE TAJIRI AMBAYE UMEJIWEKEZA VYA KUTOSHA... Ebu waza hili
Mbona sisi mzee wetu watoto wake wa 4 wamisho kuzaa kawazaa akiwa na miaka 35, 9
39, na sasaiv ni wakubwa na Wana watoto
 
Hili la mtoto lishaanza kunitoa nje ya reli

Nina miaka 28 sasa na ni mtoto wa kwanza,tupo wa4,wa3 wa kiume mmoja wa mwisho ni wa kike

Juzi Tu hapa sikukuu ya pasaka rafiki yangu niliyesoma nae kuanzia la 1 Hadi form 4 kaenda home kijijini Kula sikukuu na familia yake


Niliwaza sn maana sioni dalili ya kuoa wala kuwa na familia maana akiki yangu ipo bize kukimbizana na ndoto

Yaani sioni dalili ya kumletea bi mkubwa mjukuu labda demu anitegeshee nimpe mimba

Kumbe Tupo wengi
 
Wewe unawaza kustaafu tu, kwani kila mtu ameajiriwa hadi awaze kustaafu miaka 60?

Lakini pia kwani kustaafu ndio kufa? Kwamba ukistaafu huwezi kua na shughuli nyingine ya kukuingizia kipato na ukaendelea kusomesha ama kusaidia wanao?

Yaani wewe huoni maisha baada ya miaka 60?
We mjamaa utengenezewe sanamu la ukumbusho. Una hoja za kufikilika sana
 
Umejiandaa vipi katika makuzi yake na malezi pia sio unatoa kitu unampeleka kwa Bibi mtoto mlee mwenywe.

Unajua wanaotoa Ushauri ni Kama wale Motivational Speakers Wanasema Ukitaka Kuwa Tajiri....Mfanyabiashara Maarufu fanya A,B,C....Wakati yeye ni Kapuku!
Hatutaki Maisha ya Kumtesa Mtoto...
Suala Sio Kuzaa ukiwa na Umri Mdogo!
Issue ni
1.Uwezo wa Akili ya Kumlea Mtoto na Kuishi na Mwanamke
2.Uwezo wa Kifedha wa Kumlea Mtoto...Unakuta Mtoto Tangu yupo Mjanzito Mama anahangaika Sana na Ujauzito wake...Hapati lishe sahihi,Matokea yake Mtoto anazaliwa Na Matatizo,Kiafya,akili,Nk
Tena wengine akishazidiwa anampeleka Kwa Bibi yake....
Jamani Tafuteni Hela Kwanza Mwanaume Hakuna Kuchelewa....unakimbilia wapi?
3.Ukizaa Akili Ikiwa Imekomaa Mtoto atakuwa na Akili sana na Afya!
Afya ya akili...Ukiwahi Kuzaa Ndio maana watoto wanakuwa too much mcharuko..Akili bado haijatulia,
Na Mtoto anakuwa hivyo hivyo!
To me angalau...angalau Umefikisha 31 kuendelea ndoa Uzae...
Akili Imetulia...
Kichwa kimeshatumika kiko Vema toka Kazini,Mtaani,Kiroho,Kijamii.
Umeweza Kupambana na Kukomaa na UVUMILIVU!
Hii Ni Kwa Mwanaume!
Mwanamke the Earlier the better due to biological reason!
 
Mimi na fanya kaz na Waitaliano wanaingiza 2ml per day.. Coz wanamiliki restaurant na Hotel ... Lkn hawa jamaa Mume ana miaka 45 na mke 38 lkn hawana mtoto na hawataki kusikia kuhusu mtoto na ukiwauliza kwann wanasema mtoto ni stress kwasababu anahitaji huduma nzur na matunzo mengi.... wanasema hvyo na wakat wanaingiza pesa nying sana kwa mwez....
Na isitoshe wakisikia ww mfanyakaz una mtoto mmoja au wawil na unataka kuongeza wanakuonea huruma wanasema kuwa makin maisha magumu watoto weng watakusumbua kama unae mmoja bas anatosha usiongeze tena...

Lkn ukitizama kuna utofautmkubwa wa Kifikra kati ya mtu mweusi na mtu mweupe...!!?
 
Naona umri mzur wa kuzaa mtt wa mwisho ni miaka 40 ukifika 60 mtt wako wa mwisho ana 20 na yuko chuo ww hapo unacheza a wshukuu tu tena mambo ya baba babu co mazur na yauwa haraka sana
 
Mi naona ni majaliwa ila kwa mwanamke isizid 32 inaweza kumpa mawazo sana kama mtu anapenda watoto

Hakuna tunachobaki nacho mileleni starehe za dunia tu tutaacha kama maisha ni mpango wa mungu na rizki hutoa yeye kwa nn tuwe na wasiwasi na kitu kidogo kama icho imani zenu bado zina matatizo

Kila kitu ni mpango wa mungu wapo wakina lady jaydee na wema watu wanawasakama sio fresh sio rizki kwao waache waishi tu
 
Mtoto wa kwanza inavyosemekana ndio kila kitu kwa maisha yako ya hapo baadae. Inapotokea umechelewa kupata mtoto wako wa kwanza, huko mbeleni kuna changamoto kubwa sana za kimaisha zinaweza kukupata umri unaopochelewa kupata mtoto.

Hebu leo tujaribu kujuzana ni umri gani hautakiwi uwe umeuvuka bila ya kupata mtoto wako wa kwanza.

21-24
25-30
30-35
35-40

Ni upi umri sahihi?


Mkuu kuoa/kuolewa ni lazima ila kupata mtoto ni mapenzi ya Mungu
 
Maisha hayana formulae lakini ukimpata 21-24 baada ya first degree na ajira una uhakika wa kumtunza vizuri. Yaani uhakika wa kodi ya nyumba, mshahara wa dada, chakula, bima ya afya nk.
Hahahahahah ni idea nzuri ila kwa wale walioko miongoni mwa raia 20,000 ambao wanawania kinyang’anyiro cha PCCCB ina maana ukihangaika na kazi hupati ina maana usizae?

Mi naona kijana mwenzangu ukifika miaka 30 tafta mwanamke mwenye kazi wa kufa nae tu kiume unatia mimba life linaendelea. Mtoto mtasaidiana kulea tu kimazabe.
 
Back
Top Bottom