Elections 2010 Ni ukweli ukiweka picha ya JK kwenye gari huguswi na matrafiki?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wana-JF—Nimeipata hii mpya leo. Eti ukiwa na gari lako hapa jijini, ukabandika picha ya JK (ile yake ya smiling face yenye maandishi Chagua Kikwete Chagua CCM) hawa manjagu wetu hawatakupiga bao – kwa maana ya kukusimamisha barabarani hata ukiwa umetenda kosa gani?

Nasikia hii ni zawadi maalum kutoka CCM kwa traffic offenders na itatumika hadi Okt 31!

Yaaani Mara Mia niweke picha chakubanga kwenye gari langu kuliko ya jk
 
Believe me, kuna watu wataiba na kuua wakiwa na bango hilo la picha. Imewahi kutokea Mwanza mabatini, majambazi walijipanda kama gwaride wakatembea wanaimba usiku wa manane, "Chama Chetu cha Mapinduzi, chajenga nchi..".
Walinzi wa ghala wakazubaa na kukutwa kwenye lindo, wakakamatwa na kunyanganywa kila kitu, ghala likabomolewa na kila kwishney!
 
Ni kweli hiyo mbinu ya kubandika picha ya mgombea wa CCM inatumiwa na madereva wa maroli na madaladala.
Hawapigwi bao wala kusimaamishwa simamishwa kama zamani.
Wanachofanya maaskari ni ujinga, nidhamu ya uoga na kujipendekeza.
 
Wana-JF—Nimeipata hii mpya leo. Eti ukiwa na gari lako hapa jijini, ukabandika picha ya JK (ile yake ya smiling face yenye maandishi Chagua Kikwete Chagua CCM) hawa manjagu wetu hawatakupiga bao – kwa maana ya kukusimamisha barabarani hata ukiwa umetenda kosa gani?

Nasikia hii ni zawadi maalum kutoka CCM kwa traffic offenders na itatumika hadi Okt 31!

Sema tu sina gari. Ningekuwa nalo ningebandika picha ya chupa za mkojo zinazotupwa barabarani na walalahoi, kwa sababu hazina tofauti na picha unayoizungumzia.
 
Mtumikie kafiri upate mradi wako - Hivi inapatikana wapi hiyo picha?
 
Nimeweka stika ya chagua Dr Slaa na trafiki alipoiona alitabasamu na kuniambia nenda bwana na huku naondoka akanipigia vidole viwili.
 
Wana-JF-Nimeipata hii mpya leo. Eti ukiwa na gari lako hapa jijini, ukabandika picha ya JK (ile yake ya smiling face yenye maandishi Chagua Kikwete Chagua CCM) hawa manjagu wetu hawatakupiga bao – kwa maana ya kukusimamisha barabarani hata ukiwa umetenda kosa gani?

Nasikia hii ni zawadi maalum kutoka CCM kwa traffic offenders na itatumika hadi Okt 31!

Hata ile bendera ya CCM! Mbona hii ni kawaida kila wakati wa uchaguzi.
 
Wana-JF—Nimeipata hii mpya leo. Eti ukiwa na gari lako hapa jijini, ukabandika picha ya JK (ile yake ya smiling face yenye maandishi Chagua Kikwete Chagua CCM) hawa manjagu wetu hawatakupiga bao – kwa maana ya kukusimamisha barabarani hata ukiwa umetenda kosa gani?

Nasikia hii ni zawadi maalum kutoka CCM kwa traffic offenders na itatumika hadi Okt 31!

Kama unasumbuliwa sana na hawa jamaa wewe beba coffin hata la mtoto....wala hawatakuangalia
 
Nimeweka stika ya chagua Dr Slaa na trafiki alipoiona alitabasamu na kuniambia nenda bwana na huku naondoka akanipigia vidole viwili.

Hebu ntumie PM unieleze naipata wapi hiyo picha! Si Trafiki wote ambao wako upande wa CCM. Tena ni wengi ambao HAWAIPENDI. Ila wanaogopa kuwakamata wanaoweka hizo picha za JK, kwa kuwa kwa sasa JK amekamata dola. Wanasubiri atoke ili wamsindikize kwa matarumbeta pale Ikulu. Nasikia, eti, bendi ya Polisi inafanya mazoezi - ile ya matarumbeta, si ile Jazz band - ya kumsindikiza JK akitoka Ikulu, na kumkaribisha Slaa! Patakuwa hapatoshi! Hahahaha!

Anyway, hizi ni nyepesi tu... lakini huenda zina ukweli ndani yake!
 
Back
Top Bottom