Ni ukweli kwamba elimu yetu iko chini, ili kuokoa kizazi kijacho tufikirie mabadiliko

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,017
2,154
Mtoto rafiki yangu alisoma kwao Ghana, alifaulu vuzuri six form na sasa amepata nafasi ya kusomea u daktari Ulaya. Kutokana na unafuu wa ada amempeleka Poland na ana mudu kumljpia ingawa rafiki imebidi akate starehe nyingi tu.

Mtoto alipata alama za juu sana, kila chuo alichopeleka maombi aliitwa kwa usail au kupewa nafasi. Nilimuuliza siri ya mafanikio hayo. Aliniambia licha ya kuwa mtoto ni mwepesi kueleww lakini shule aliyompekeka tangu akiwa form one ni nzuri sana.

Hiyo shule walimu wake wengi wametoka India,,walimu wa Ghana wanaofundisha hapo ni wale walio na experience ya miaka kumi au zaidi na wana sifa za ziada. Mshahara wa walimu unaanzia US $ 1,500 kwa mwezi na free accommodation unachangia utility bills tu. Mwenye shule alijenga flats karibu 50 wakati wa ujenzi wa shule kwaajili ya wafanyakazi.

Nilikumbuka kusoma malalamiko humu juu ya viza za walimu wa nje wanaokuja kufanya kazi Tanzania. Kama tunataka kusonga mbele turuhusu walimu wageni, hata kama ni watoto 500 watapata elimu bora hao wataelimisha wengine 5000 kwa kizazi kijacho.
 
Back
Top Bottom