Ni ukomavu wa kisiasa m-CCM kuwatia shime upinzani

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,817
35,827
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Inavutia Colin Powell a staunch republican 'kum' endorse Joe Biden a staunch Democrat kwenye uchaguzi ujao:

Colin Powell: 'Biden will be a president we will all be proud to salute'

Jamani eeh upinzani si ugomvi. Hata huko CCM kutoa hisia zenu za moyoni wazi wazi si uhaini.

Mabadiliko kwa sasa ilikuwa ni muhimu na muda muafaka sana. Hii ikiwa mahsusi kabisa kuwatia adabu miungu watu wachache wanaojaribu kutupeleka kusiko.

Hii nchi haiwezi kuwa mali ya mtu binafsi kufikia tulikofikishana. God forbid! Mifano ni mingi na lukuki mno.

Siasa za vyama kupishana kila inapobidi ni kichecheo cha maana mno kwa maendeleo ya taifa lolote.

Vyeo ni dhamana, hii nchi ni yetu sote.

Maendeleo si mali ya chama fulani.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Usifananishe Kenge na Mamba

Mkuu kenge na mamba wote ni amphibians tu.

Kuyatambua mambo ya msingi kwa wagombea na kuwatunuku vilivyo hakupaswi kuwa kishabiki shabiki tu.

Endorsement ni moja ya mambo ya afya katika kuweka maslahi ya taifa mbele.
 
Back
Top Bottom