Ni ukomavu wa hali ya juu, taifa letu limeonesha kuwa hakuna aliye juu ya sheria

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Ibara ya 13(6)(a-e) imeeleza wazi uhumimu wa haki ya kila mtu anayetuhumiwa kufanya makosa kutendewa haki mbele ya mahakama na vyombo vya usalama.

Haki hizi ni pamoja na kutopata mateso kwa watuhumiwa wakiwa chini ya vyombo vya dola. Kufikishwa mahakamana kisha kusikilizwa na kutiwa hatiani bila kuonewa.

Taifa letu limeshuhudia watu wa kila namna, maskini, matajiri na wanasiasa wakipandishwa vizimbani.Hii ni ishara kuwa sheria zinazingatiwa.

Harbinder Seth, Amber Lutty Ndama Mutoto ya Ng'ombe , Freeman Mbowe na wengine wengi wamefikishwa kizimbani.

Huu ni mfano mzuri. Taifa letu linafanya vizuri.
 
Ukomavu upi unaoongelea hasa???

Paul Makonda mbona yupo juu ya sheria, hulioni hilo, au una makengeza ya akili. Acha kujifanya kichaa.

Makosa ya Jinai aliotenda yalio wazi kabisa katika Penal Code CAP 16 [PRICIPLE LEGISLATION] ni mengi sana, kufikia hatua mpaka baadhi ya Wakuu Wa Wilaya walikua wakimuiga kutenda makosa hayo (Ref: Ole Sabaaya alikua anawauliza wafanyabiashara kwamba mnataka twende Makonda Style?). Ila Makonda hakuwahi kufikishwa mbele ya mahakama.

1) Armed Robbery Contrary To Section 285, 286 and 287 - Ujambazi Wa Kutumia Silaha, aliingia kwenye ofisi za watu bila idhini, kwa nguvu na kwa kutumia silaha za moto kuchukua mali za ofisi bila consent za wahusika.

2) Kidnapping and Abduction Contrary To Section 244 & 246 - Utekaji nyara, Alishiriki kuteka watu (Ref: Issue ya Mo Dewj na Roma Mkatoliki).

3) Misuse Of Authority Of Office Contrary To Section 96 - Alitumia vibaya madaraka yake na Ofisi za umma kwa kubambikiza watu kesi za madawa ya kulevya na kuwanyang'anya mali zao, zikiwemo gari na fedha kwa kutumia cheo na ofisi yake.

Hayo ni baadhi tu ambayo kwa uchache angekula mvua ya Miaka 60 jela na kwenda mbele.

Huyu hayupo juu ya sheria??? Ndio ukomavu wenyewe unaosema???
 
Paul Makonda mbona yupo juu ya sheria, hulioni hilo, au una makengeza ya akili. Acha kujifanya kichaa.

Makosa ya Jinai aliotenda yalio wazi kabisa katika Penal Code CAP 16 [PRICIPLE LEGISLATION].

1) Armed Robbery Contrary To Section 285, 286 and 287 - Aliingia kwenye ofisi za watu kwa nguvu na kwa kutumia silaha za moto kuchukua mali za ofisi.

2) Kidnapping and Abduction Contrary To Section 244 & 246 - Alishiriki kuteka watu akiwemo Mo Dewj na Roma Mkatoliki.

3) Misuse Of Authority Of Office Contrary To Section 96 - Alitumia vibaya madaraka yake na Ofisi za umma.
Hoja yako nini hasa?
 
Mkuu mbona unamhukumu kama wewe ni mahakama?
Kichwa chako cha habari kinasema ni ukomavu wa hali ya juu kwa taifa letu kuonesha hakuna mtu alie juu ya sheria. Nlichoandika ni kupinga kauli yako hio, kwamba kuna watu wametenda jinai ila hawakufikishwa mbele ya hizo mahakama (Meaning to, wapo juu ya mahakama).

Hizo ni hoja kijana umejibiwa. Acha kulalama.

Hakuna cha ukomavu katika taifa letu, sheria na mahakama zipo Double Standard - Kwa baadhi watafikishwa mahakamani ila wengine hawatafikishwa mahakamani.
 
Kichwa chako cha habari kinasema ni ukomavu wa hali ya juu kwa taifa letu kuonesha hakuna mtu alie juu ya sheria. Nlichoandika ni kupinga kauli yako hio, kwamba kuna watu wametenda jinai ila hawakufikishws mbele ya hizo mahakama (Meaning to, wapo juu ya mahakama).

Hizo ni hoja kijana umejibiwa. Acha kulalama.

Hakuna cha ukomavu katika taifa letu, sheria na mahakama zipo Double Standard - Kwa baadhi watafikishwa mahakamani ila wengine hawatafikishwa mahakamani.
Sipendi kuhukumu mtu. Ila tambua kuwa jinai haina Mwisho.
 
Back
Top Bottom