Ni ujinga uliopitiliza kupanga foleni kumpigia kura mgombea wa CHADEMA/upinzani wakati msimamizi wa uchaguzi ni kada wa CCM

Kumbe sisi wananchi katiba haina manufaa kwetu ni kwa manufaa ya wanasiasa wa upinzani tu kushinda chaguzi?
 
Leo umeongea kitu muhimu sana mzee baba hebu agiza pisi moja ya bange nitalipa..

Ni hivi upinzani bongo mi mchezo wa kuigiza mwaka jana walisusia uchaguzi wa serikali za mitaa ila mwaka huu wako tayari kugombea ubunge,diwan na urais lakini hawajasema kama kile walichokikataa mwaka jana kimebadilishwa au la..kiufupi kwa sasa siwaelewi wanachokisimamia na hapo ndo CCM wanapata upenyo wa kutupiga bakora.
 
2025 Dr Magufuli atakuwa wapi?
Tatizo wapinzani au ccm wanahisi watanzania hawaoni hata yanao endelea ccm kuna wachumia tumbo wengi tena majizi yamejificha kwenye mgongo wa chama dola. Wapinzani wameamua kuwa vibaraka wa mabeberu mchana kweupe. Tanzania tumebaki na magufuli muda wake ukiisha Mungu atatuletea mwingine wa kutuongoza kwasasa option ni moja tu ieleweke hivyo
 
Kaka tukubali kupokea ukweli mchungu hata kama unatuumiza kiufupi jamaa amesema kweli Pale Nec kila kitua anateua Rais unategemea nini? Na mara kwa mara alishawapiga mikwara iwapo watatangaza mpinzani
Zote hizo ni janja zetu za kuzuia watu wasipige kura kwa kuwatia fear of unknown ili mpate nafasi ya kuiba tofauti na wengi wakipiga kura watawapa kazi jinsi ya kutally wizi wa kura.Huwezi jua msimamizu anaweza jazwa Roho Mtakatifu pia.
Watu wajitokeze kwa wingi wao ndio waamue wawatakao.
 
mwenyekiti wa chadema na mkuu wa chama ndani ya ACT hivi walipatikanaje? Tenda haki ndio udai haki! Kunawatu waliambiwa sumu haionjwi kwa ulimi.
 
Wananchi ni lazima tujue kwamba katiba ya JMT ndio inayobariki ushindi wa CCM.

Na kiukweli ukiangalia maeneo ambayo upinzani huwa unashinda mara nyingi inakuwa ni ulegelege wa mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi au huruma tu ya CCM yenyewe.

Ni wale wananchi wapenda mageuzi mkaendelea na shughuli zenu nyakati za uchaguzi hadi pale hawa wanaojiita wapinzani watakapoipambania kwa dhati katiba mpya.

Kwa sasa wapinzani hawa uchwara wanapambania ruzuku ndio maana malengo yao wote ni kuwa " chama kikuu cha upinzani"

Maendeleo hayana vyama!
Mataga Leo akili imerudi.yuko pamoja. Kuanzia Leo wewe ndio mataga kwenye akili timamu
 
Ukweli mchungu, nccr Ni mfano halisia.wanapambana kuwa chama kikuu cha upinzani badala ya kuwa chama tawala.kwa tume hii ccm ushindi Ni lazima
 
Wananchi ni lazima tujue kwamba katiba ya JMT ndio inayobariki ushindi wa CCM.

Na kiukweli ukiangalia maeneo ambayo upinzani huwa unashinda mara nyingi inakuwa ni ulegelege wa mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi au huruma tu ya CCM yenyewe.

Ni wale wananchi wapenda mageuzi mkaendelea na shughuli zenu nyakati za uchaguzi hadi pale hawa wanaojiita wapinzani watakapoipambania kwa dhati katiba mpya.

Kwa sasa wapinzani hawa uchwara wanapambania ruzuku ndio maana malengo yao wote ni kuwa " chama kikuu cha upinzani"

Maendeleo hayana vyama!
Ni Polepole amekutuma “KUENEZA” hii habari?! Mna mapenzi ya dhati na CDM na upinzani kwa ujumla! Asanteni sana!
 
Back
Top Bottom