Ni uhuru upi wa kujieleza wanaoutaka CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Jikite kwenye hoja kamanda acha kuweweseka
Mimi si CHADEMA. Si lazima uwe CHADEMA kuhoji kuhusu uhuru.

Hata mimi nilihoji.

Tuanze na swali hili.

Magufuli alivyopiga marufuku mikutano ya kisiasa alitumia kifungu gani cha sheria?
 
Kuna dhana potofu ambayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekuwa wakiwaaminisha Watanzania eti hakuna uhuru wa habari na vyombo vya habari vimeminywa. Dhana hiyo imekuwa ikiwashangaza hata waandishi wa habari wenyewe kwani hawajaona kuminywa huko kwani wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira rahisi kuliko wakati wowote.

Ni Chadema hao hao wanaolilia uhuru wa habari wakati wao wenyewe wamekuwa wakiuminya kwa kufanya vitu ambavyo vimewawia vigumu hata wanahabari kutekeleza majukumu yao wakiwa nao kwa kuhofia usalama wao. Suala hilo linatokana na ukweli kwamba wakati wa uzinduzi wa kampeni zao pale Jangwani jijini Dar es Salaam, Chadema waliwatimua bila huruma waandishi waliokuwapo hapo wakitekeleza majukumu yao kwa madai kuwa wamewahujumu.

Ukiambiwa hawa watu wana akili fupi nadhani utaelewa nini namaanisha; unawezaje kumtimua mwandishi ambaye chombo chake kinaripoti moja kwa moja ‘live’ tukio hilo na wewe hapo hapo unamtimua huku ukihamasisha wafuasi wako wawapige ili kuwaongezea mwendo wa kutoka eneo hilo.

Kama kawaida yao hawakukomea hapo, katika ilani yao ambayo kwa asilimia 95 wamechukua mambo yaliyopo kwenye katiba na kuahidi kuyatekeleza lakini wakiwaaminisha Watanzania ni matarajio na vipaumbele vyao watakavyofanya wakishika dola.

Katika ilani yao Ukurasa wa 18, wameandika: Kwa kuwa Chadema inaamini katika fikra huru na mawazo mbadala kama msingi wa ujenzi wa uchumi shirikishi na hivyo kuleta maendeleo endelevu katika taifa; hivyo basi, Serikali ya Chadema itafanya mambo yafuatayo katika eneo la uhuru wakujieleza:-

a. Itahakikisha kwamba kila mwananchi anakuwa na uhuru kamili wa kueleza fikra zake, kupata na kutoa habari, kukusanyika na kujiunga na kikundi au chama chochote kwa hiari na utashi wake.

Hivi leo kusingekuwa na uhuru wa watu kujieleza watu wangekuwa wanapata wapi taarifa/habari za makundi ya watu na mtu mmoja mmoja kama wanasiasa, madaktari, wafanyabiashara, waendesha bodaboda, mama lishe nk? Kusingekuwa na uhuru wa kukusanyika, wangefika walipo sasa? Kusingekuwa na uhuru wa watu kujiunga na kikundi au chama leo hii kusingekuwa na utitiri wa vyama vya siasa, vyama vya kuweka na kukopa (Saccoss) au vyama mbalimbali vyenye mlengo tofauti ambavyo vimesajiliwa kwa mujibu wa sharia. Ni kwa sababu uhuru huo upo ndiyo maana

b. Itahakikisha kwamba, vyombo vyote vya habari; vya umma na binafsi, vinakuwa na uhuru wa kutafuta na kutoa habari bila upendeleo. Hili nalo ni tatizo jingine ambalo Chadema wameamua kujifanya hawalioni au huenda hawalijui.

Vyombo vya habari havijawahi kukosa uhuru wa kutafuta na kutoa habari ndiyo maana taarifa katika magazeti, Televisheni, radio, blogu na vyombo vingine zinafanana kimatukio kulingana na wakati na nyingine hazifanani. Na hii kwa sababu tu kila mtu/chombo kinatafuta habari kwa namna yake ili mradi hakivunji sheria. Sheria inavyosema kuhusu uhuru kutoa maoni na kupata habari Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inasema:

(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Hayo ni mambo yaliyopo kisheria na yameendelea kutekelezwa tangu uhuru, sasa ni uhuru gani wanaoutaka Chadema, au wa watu kuwaoza watoto wao wa kiume kwa wanaume wenzao?

mpaka leo sjaelewa huo uhuru wanaoutaka maaana jamii forum apa kila mtu yuko huru kuelezea maoni yake lakini mpaka leo sjaona cha maaana walichoongea zaidi ya kusubiria matukio ili waanzishe uzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom