Ni Udikteta kulazimisha Waziri Mkuu kuteuliwa miongoni mwa Wabunge wa kuchaguliwa. Ni kichekesho Waziri Mkuu kuidhinishwa na Bunge

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,205
4,695
NI UDIKTETA KULAZIMISHA WAZIRI MKUU KUTEULIWA MIONGONI MWA WABUNGE WA KUCHAGULIWA

NI KICHEKESHO WAZIRI MKUU KUIDHINISHWA NA BUNGE

UTARATIBU WA WAZIRI MKUU KUWA NA MANAIBU WAWILI UANZISHWE

Wadau

Nitazungumzia hoja mbili kwa ufupi kuhusu utaratibu wa uteuzi wa Waziri Mkuu na umuhimu wa kuwa na Naibu Waziri Mkuu wawili

Nitoe maoni yangu mchakato unaotumika kumpata Waziri Mkuu unaolihusisha Bunge haufai, umepitwa na wakati, ni kichekesho, ni udikteta, ni upuuzi na hauna matokeo chanya kwa nchi yetu.

Nasema utaratibu huu haufai hata kidogo kwa sababu

Unazuia Watu wenye sifa stahiki na uzoefu mbalimbali kukosa fursa hiyo muhimu kwa kuwa sio Wabunge na hivyo kuikosesha Serikali na Watanzania fursa ya kuhudumiwa kikamilifu na mtu mwenye sifa stahiki.

Nitoe ushauri pia upo umuhimu wa kuanzisha utaratibu wa Waziri Mkuu kuwa na Wasaidizi wawili ( Naibu Waziri Mkuu) ili kurahisisha utetekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Kiserikali pamoja na kuongeza uwajibikaji

Waziri Mkuu & Manaibu wake wateuliwe kutokana na sifa zitakazoainishwa na sio lazima watoke miongoni mwa Wabunge ila watakapoteuliwa waingie bungeni moja kwa moja.

Ni vema pia Watendaji hao Wakuu wa Serikali wakapewa majukumu kwa mkataba maalumu ambao utaongezwa kwa kuzingatia matokeo ya utendaji kazi kulingana na majukumu waliyokabidhiwa
 
Back
Top Bottom