Ni "udhaifu" kwa mwanataaluma hujidhalilisha/kudhalilika kwa sababu ya siasa

Labrujita

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
399
126
Ndg wana JF nawasalimu kwa jina la Bwana.

Sote tunatambua namna ambavyo siasa imekuwa na nguvu na inavyotawala kila kitu. Inadhaniwa ya kwamba utamu ulioko kwenye siasa ndio ambao umekuwa chanzo cha wanataaluma wengi kukimbia taaluma zao na kuamua kujitosa kwenye siasa mahali ambapo wengi wao wamejikuta wakibadilika aidha kwa kutaka wenyewe au kwa kubadilishwa kwa style ya kuendana na mfumo au matakwa ya chama au serikali.

Mara nyingi weledi wao, akili zao, uzoefu wao katika kutafuta suluhu ya matatizo kwa mantiki ya evidence based ni kama huwa wamefungia nyumbani na kuamua kutumia njia nyingine katika kuzitumikia nafasi zao za kisiasa. Kwa misingi hii inafika wakati imani juu ya wanataaluma wetu katika kusaidia ujenzi wa taifa inakuwa haipo kwani kukubali kubwaga slaa zako chini na kubaki mataka uliyefungwa kitambaa kichwani maana yake umekubali kutumika. kukubali kutumika ndio mwanzo wa ulafi, umimi na mengineyo mengi yasiofaa ndani ya jamii na ni jambo ambalo mara nyingi huwaondolea hazina ya heshima waliyokuwa mwanzo.

Nachelea kutoa mfano mmoja tu wa wanataaluma waliokataa utumwa kwa gharama ya kulinda heshima na taaluma zao; kama aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati wa mchakato wa katiba mpya namna alivyojitoa sadaka kuitetea taaluma yake, angalia heshima aliyo nayo PLO Lumumba mara baada ya kufukuzwa katika taasisi ya rushwa nchini Kenya na mifano mingine mingi.

wanataaluma wetu hususani mlioko katika siasa tafadhali sana tunaomba ile dhana ya "elimu ni kwa ajili ya ukombozi" basi muitumie hivyo na mjiepushe kuwa mifano mibaya kwa jamii kwani kuzitumia taaluma zenu kinyume na inavyotakiwa ni kulidhuru taifa. Tunakoelekea kuna hatari pengine ya neno "uchwara" kutumika kutugawa katika makundi mawili kwa maana ya mwanataaluma uchwara, mwanasheria uchwara au kama wewe ni profesa kuitwa profesa uchwara. Nawasilisha
 
"elimu ya mtanzania hutumika tanzania kwa kuididimiza tanzania"...


"siasa za tanzania hufanyika tanzania kwa kuwadidimiza watanzania"...
 
hivi ni kweli Ibrahimu Haruna Lipumba aliwahikua mgombea urai waTz kwahii move alotuonyesha uraisi angeuweza?
 
Back
Top Bottom