Ni uchizi kutenga bilioni 10 tu kuondoa foleni dsm

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Jana nilipata bahati ya kusikiliza marudio ya hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe John Mnyika iliyosababisha atolewe nje ya ukumbi, wakati akitolewa nje Mhe John Mnyika alikuwa akisisitiza kuwa licha ya wabunge wa CCM kujigamba kuwa bajeti inazingatia Ilani ya CCM lakini "Mzimu upo katika maelezo" the "Devil is in the details" kwani ukisoma bajeti unakuta vitu vya "KICHIZI KICHIZI TU" kama vile kiasi kidogo cha Shs Bilioni 10 tu kutengwa kuondoa tatizo la foleni katika Jiji la Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa upo mpango wa kujenga barabara mbali mbali kuzunguka Jiji la Dar es Salaam kwa kiwango cha lami ili kuwawezesha madereva wa magari kutumia barabara mbadala badala ya barabara chache kubwa zilizo katika hali nzuri k.m barabara za Morogoro, Bagamoyo, Sam Nujoma, Ali Hassan Mwinyi, Ilala, KIlwa Road, Morocco n.k za zingine chache. Kutokan ana barabar hizi chache kuwa katika hali nzuri, magari hulazimika hujirundika huko kutokana na barabara zingine zote kuwa mbovu sana na kutpitika hata wakati wa kiangazi. Licha ya kupitika kwake barabar hzi ni nyembamba na hivyo kuchangia kuwepo kwa msongamnao mkubwa wa magari.

Vitu vya kichizi kichizi alivyodai Mhe John Mnyika ni kama vile matumizi ya kawaida yametengewa trilioni 10.5, sawa na asilimia 70, na matumizi ya maendeleo yametengewa trilioni 4.5, sawa na asilimia 30, wakati fedha za ndani zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni trilioni 2.2 tu, badala ya 2.7,” kama inavyoelekezwa na Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 uliopitishwa na bunge na kuwekwa sahihi na Mheshimiwa Rais.


Hivyo sio haki kabisa kwa tatizo la foleni katika Jiji la Dsm kutengewa Shs Bilioni 10 tu ilihali wakazi wa Jiji hili huchangia zaidi ya 80% ya makusanyo yote ya ndani kwa maana ya Kodi. Hivyo kati ya makusanyo hayo Shs trilioni 1.2 zitatoka katika jiji hili. Wakati wakazi Jiji la DSM wakikesha katika foleni matumizi ya kawaida katika bajeti yakipanda kwa trilioni 1.9 wakati fedha za maendeleo zikipungua kwa bilioni 397.8 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2011/12;

Laiti kama Serikali ingekuwa inazingatia vipuambele vya taifa hili na kuwasikiliza ingekubali kuzingatia Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano ulipitishhwa na kutenga trilioni 2.7 badala ya trilioni 2.2 ambayo ingeleta ongezeko la sh bilioni 500 katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuondoa foleni katika Jiji la Dar es Salaam.

Je ni kwanini Serikali isikubali hizi Shs Bilioni 397 zisitumike kutengeneza barabara za kuzunguka Jiji la Dar es Salaam kama vile Bunju-Mbezi-Ukonga; Mbezi Juu-Mbezi Luisi-Ukonga na zinginezo zitakazotumiwa na magari ili kupunguza magari katika barabara chache za Jiji hili kwa lengo la kupunguza muda wakazi wa DSM wanaoutumia mabarabarani kila asubuhi na jioni ili waweze kuzalisha zaidi na hivyo kulipa kodi zaidi?

Je huu sio uchizi na udhaifu mkubwa kwa watu wenye na chama chenyz dhamana ya kuongoza nchi kuyakataa mapendekeoz kama haya na kuendelea kutenga fedha nyingi kwa aili ya safri za nje na kulipana posho?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom