Ni ubalozi au ubalazuli?

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
532
Ubalozi wa nyumba kumi una umuhimu mkubwa sana ukitumiwa vizuri. Balozi anagusa wananchi kuliko rais wa nchi.

Tatizo ni kutotambuliwa umuhimu wa hii kazi. Mabalozi wengi wanaishia kwenye kuamua kesi za ugoni na kusambaza ubuyu (umbea). Ubalozi wa hivyo si ubalozi ni ubalazuli (baradhuli)

Kama wewe ni balozi na mtaa wako hauna
kibao cha jina wewe ni balazuli.

Kama wewe balozi na nyumba za mtaani kwako hazina namba wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako gari la taka halipiti wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna madimbwi ya maji wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako hakuna mifereji iliyozibwa ya kupitisha maji ya mvua wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna vijiwe vya bangi na mateja wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna danguro la changudoa wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na huna orodha ya wakazi wa mtaa wako wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna kibaka au jambazi anaejulikana wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna mtu anapiga mkewe wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna mtoto haendi shule wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna walokole wanatumia vyombo vya muziki wa dansi kubughudhi wakazi wa mtaa wakiwemo wagonjwa, wazee na watoto wachanga wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako kuna mijibwa na paka wasio na mwenyewe wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako maji hayatoki wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na mtaani kwako baa hazifungwi wewe ni balazuli.

Kama wewe ni balozi na huna kamati ya utendaji wewe ni balazuli.

Hayo na mengine mengi yanaweza kudhibitiwa na balozi na kamati yake utendaji. Balozi anaweza kutoa amri wakazi washirikiane kuchimba mfereji wa maji. Ikibidi kulipia balozi anaweza kukusanya pesa za kulipia gari la taka. Asieweza kulipa ahame mtaa. Msione miji ya watu ni misafi wakazi wanalipishwa kuisafisha na wanawajibika kufuata sheria za miji.

Balozi anatakiwa atinge sana kwenye vyombo vinavyohusika kuhakikisha huduma za jamii zinafika mtaani kwake hata ikibidi kuripoti magazetini na redioni.

Balozi usibishane na watu wala huhitaji vikao vingi. Na huhitaji kuwaandikia watu barua za kijinga eti waje nyumbani kwako kujadili halafu hawaji. Bandika tangazo kwenye kila mlango wa mkazi ueleze kinachotakiwa kufanywa atakebisha peleka polisi.

Polisi watafurahi sana kuongezewa kesi wawapige watu faini na ikibidi wawafunge jela.

Mitaa itakayokuwa na mabalozi wazuri itakuwa misafi, uhalifu utapungua, maradhi yatapungua, watoto watasoma na watakuwa na nidhamu na bei za nyumba zitapanda.
43b0bde4d5b67eb6597e99ecc60658be.jpg
 
Huyo ni balozi changamoto kwenu madiwani, katibu tarafa, meya na wakuu wa mikoa. Maendeleo huletwa na serikali za mitaa.
 
Kwenye miaka ya nyuma kuna mkuu wa mkoa Morogoro alifanya kampeni ya usafi mji ulikuwa msafi kama paka.
 
Back
Top Bottom