Ni tume huru ya Uchaguzi au Katiba mpya?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,159
2,000
Wakuu hebu tuliweke sawa hili!

Hivi tunapolilia tume huru ya Uchaguzi bila katiba mpya iili mambo yakae sawa hasa wakati wa uchaguzi tunamaanisha nini? Inawezekanaje tume ya Uchaguzi iwe huru? Kwani muundo wa tume utakua chini ya nani kwa katiba ya sasa?

Kwa katiba yetu hii Rais ndiye mteule wa Viongozi wote wakuu wa tume kuanzia Mwenyekiti wake hadi wakurugenzi wote, tena mbaya zaidi kwa wakati huu teuzi za wakuu wengi wa Idara za Serikali zinaangalia makada wa CCM. Hivyo bila kumuondolea Rais mamlaka ya kua mteuzi wa maafisa wote wa tume hatuwezi kua na tume huru.

Tusililie hili bila kuliangalia kwa umakini mkubwa, mahitaji yetu ili kulibadili taifa hili ni kupunguza mamlaka makubwa yaliyoko Ofisi ya Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala.

Tume ya taifa ya Uchaguzi inatakiwa kuachana na utaratibu wa kutumia wakurugenzi wa halmashauri kua wasimamizi wa chaguzi mbali mbali nchini, viongozi hawa wengi wao ni makada wa CCM kwahiyo lazima kuwe na conflict of interest kwa kiasi kikubwa. Tume ni taasisi kubwa, iajiri maafisa wengi hasa vijana waliohitimu vyuo vikuu kwa masomo ya sheria,siasa na katiba na watapakae kila mkoa na wilaya ili kusimamia Uchaguzi. Mbona TAKUKURU wameweza, mbona taasisi zingine zilizoanzishwa hivi karibuni zina nguvu kazi za kutosha lakini NEC wanashindwaje? Au ni makusudi? Hili suala ni la kutazwa kwa nguvu zote.Upinzani nchini hebu amkeni acheni kulala na kulialia.

Ni tume au katiba? Kipi muhimu zaidi?
 
Bururu

JF-Expert Member
May 21, 2016
846
1,000

Nawashangaa Upinzani kwa nini mpaka sasa hawaoni swala la Tume huru ya Uchaguzi.Bora waachane na mengine yote wapiganie tume na katiba
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,125
2,000
UKAWA should wake up now..

Waamshe agenda moja tu hivi sasa nayo ni KATIBA mpya..

Tukishapata Katiba mpya maana yake itakuwa ina stipulate uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi..

Hapo tu ndio tutaweza kuwa na Uchaguzi huru na wa haki
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,308
2,000
MENGELENI KWETU: Kwa nini kila kitu mnataka waanzishe UKAWA? Hivi Katiba mpya ni hitaji la UKAWA au sisi watanzania kwa ujumla bila kujali itikadi za kisiasa? Huwa mnaniudhi kweli ninyi watu. Kila kitu chema ambacho ni hitaji letu sote mnawalalamikia UKAWA kwamba wamelala. Hivi wamelala wao au tumelala sisi wote? Najua UKAWA ni wanasiasa, lakini katiba ni yetu sote hata wasiopenda siasa. Wanasiasa wakiwemo UKAWA wanapaswa kusukuma mbele agenda yetu sisi au kile tunachokitaka sisi na tuanze kukidai sisi kabla ya wanasiasa.

Watanzania tumekuwa na utamaduni wa kinafiki sana! Wapinzani walipopiga kelele kuhusu Sheria mbovu za madini, kwamba sheria hizo zinatufanya tuibiwe madini yetu hatukuwaunga mkono kwa nguvu zote. Leo amekuja huyu akachukua agenda ileile ya upinzani ya kulalamika kuibiwa madini tunamshangilia na kutoa matamko ya kumuunga mkono kila kona wakiwemo viongozi wa dini ambao walikuwa kimya wakati wapinzani wakipiga kelele hadi kuwekwa rumande na kufukuzwa bungeni kwa jambo hilohilo.

Watanzania tuna matatizo makubwa ya kiakili na ukosefu wa maarifa ndiyo maana tunaangamia kila kukicha. Hebu fikiri mtu anatunga wimbo wa kwamba 'utaisoma namba', maana yake 'utaumia '. Anakuimbisha wimbo huo wakati huohuo anakuomba umpe kura akutawale. Na kwa ujinga kweli unampa kura huku ukinengua na kucheza huku ukiimba wimbo huohuo wa kuisoma namba, wimbo wa kwamba utapata maumivu kwa kumchagua anayekuimbisha wimbo. Ajabu!
 
  • Thanks
Reactions: Gut

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom